Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na
viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani,
waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa
ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo
jioni.
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur
nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla.
Miili
hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa
kumi.
Mbali
na Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, ni
pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai
Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu
Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nape Nnauye na Ridhiwan
Kikwete.
Mara
baada ya kuwasili miili hiyo iliongozwa na msafara kuelekea hospitali
ya rufaa ya Jeshi, Lugalo, kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi siku ya
Jumatatu Julai 22, 2013 itakapoagwa rasmi kwa heshima zote katika Uwanja
wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es
Salaam, ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi Mkabala na Ukumbi wa Diamond
Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.
Waandishi
wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na
hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha
wakitetea amani duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi
na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani,
waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa
ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo
jioni.
Makamu
wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd
na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam.
Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur.
Baadhi ya wananchi waliofika kupokea na kushuhudia mapokezi hayo ya miili ya mashujaa wetu.
Mama
mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya
wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye
ndege.
Mama
mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya
wafiwa akishikiliwa na wenzake wakati akilia kwa uchungu baada ya kuona
majeneza yakishushwa kwenye ndege.
Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima.
Mama
mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya
wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye
ndege.
Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo.Picha zote na OMR
No comments:
Post a Comment