Askari
saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa
katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanatarajiwa kuagwa leo kwenye
viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo.
Miili
ya wanajeshi hao iliwasili nchini juzi kwa ndege maalumu katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J. K Nyerere, Terminal One na kwenda
kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Wanajeshi
waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed
Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na
Fortunatus Msofe.
“Shughuli
ya kuaga kwa heshima za kijeshi itaanza saa tatu kamili asubuhi katika
viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga na
itaendelea mpaka mchana kabla ya kusafirishwa,” ilisema taarifa hiyo. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Wanajeshi
hao ambao ni miongoni mwa askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha
Kulinda Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan, waliuawa kutokana na
mashambulizi ya kushtukiza yaliyofanywa na waasi wanaopigana na
Serikali, hivyo kuwa ni mara ya kwanza kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa
Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kuuawa kwa wakati
mmoja.
No comments:
Post a Comment