STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel amesema amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari hivi karibuni.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Jacqueline alisema ajali hiyo ilitokea maeneo ya
Mbezi alipokuwa akielekea nyumbani kwa mama yake, Mbezi jijini Dar akiwa
kwenye gari lake dogo, aliligonga kwa nyuma gari aina ya DCM.
“Ni
ajali ya ajabu kweli niliipata, maana DCM limefunga breki za ghafla
mbele yangu na mimi nilikuwa nimejisahau nikalivaa ila namshukuru Mungu
kwa kuwa sijaumia ila gari langu tu ndiyo limeharibika vibaya kwenye
shoo ya mbele,” alisema Jacqueline.
No comments:
Post a Comment