Katibu mwenezi CCM Nape Nnauye.
Hali bado ni tete kwa makada sita waliofungiwa na CCM kujihusisha na masuala ya uchaguzi baada ya chama hicho tawala kueleza kuwa mchakato wa kuwachunguza haujakamilika na adhabu yao inaweza kuendelea hata baada ya vikao vya juu vitakavyofanyika mwishoni mwa wiki.
CCM pia imebadili tarehe za vikao vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ambavyo awali vilipangwa kufanyika Mei 20, 21 na 22 na badala yake sasa vitafanyika Mei 22,23 na 24.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za chama hicho jijini, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hafahamu lini adhabu ya viongozi hao itakwisha kwani bado mchakato wa kuwachunguza haujafika mwisho.