Friday, May 01, 2015

YANGA INA MATUMAINI YA USHINDI

 
Kocha mkuu wa Yanga Hans Pluijm.
 
Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema wana ari ya kushinda mechi yao ya mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Etoile du Sahel licha ya kuwaacha wachezaji wake tegemezi katika msafara wao wa Tunisia.

Yanga imeondoka Dar es Salaam Jumatano usiku huku wachezaji wake tegemezi, wakiwemo Hassan Dilunga, Salum Telela na Danny Mrwanda, aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchini Vietnam wakiachwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kifamilia. “Yanga imesajili zaidi ya wachezaji 20, wote ni muhimu katika timu”.

“Ni kweli niliwahitaji katika mechi yetu ngumu dhidi ya Etoile, lakini sababu mbalimbali zimepelekea kuachwa kwao”, amesema Pluijm. Yanga itacheza na wenyeji wao, Etoile du Sahel katika mechi ya marudiano ya raundi ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mechi iliyochezwa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 hivyo kuwa na kibarua kigumu cha kushinda ugenini huku wenyeji wao wakililia sare ili kucheza hatua inayofuata. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...