Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.
Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake. Taarifa
ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa
wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na
Marekani hukutana.
Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Saud Arabia imeanza operesheni zake za kijeshi nchini Yemen, ikiwa ni kujibu ombi la Rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansour Hadi. Balozi
wa Saudi Arabia Nchini Marekani amesema kuwa, taifa lake na washirika
wao wa ghuba wanatumia mashambulizi ya angani katika harakati za kuunga
mkono serikali halali ya Yemen, ili isichukuliwe na kundi wa waasi la
Houthi.
Awali duru zasema kuwa wapiganaji wa Houthi walikuwa wakikaribia kuutwa mji wa Aden, ulioko kusini mwa Nchi hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Shirikisho
la kandanda nchini Uingereza limesema lina mpango wa kuwa na mazunguzo
na Kocha mkuu wa timu ya England Roy Hodgon mapema mwaka ujao.
Hodgon
mwenye miaka 67 alipokea mikoba ya kuifundisha England mwaka 2012
kutoka kwa Fabio Capello lakini timu ikatolewa mapema katika hatua ya
makundi kwenye kombe la dunia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
JOTO la Uchaguzi wa Rais ndani ya CCM linazidi kupanda huku makada na viongozi wa chama hicho wakipigana vijembe hadharani.
Hali hiyo inatokana na kile kinachojitokeza sasa, kuibuka kwa makundi ya
jamii, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, kuwashawishi makada
kadhaa wa CCM wawanie nafasi hiyo ya uongozi wa nchi katika Uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
Makada ambao wamekuwa wakishawishiwa kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa
Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu),
Profesa Mark Mwandosya na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.
Wakati baadhi ya makada wengine wanaotajwa kutaka kuwania urais ndani ya
CCM wakimlalamikia Lowassa, wachambuzi wa siasa wamekuwa wakihoji
mpango wa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba, alipochapisha vitabu na kugawa kwa wajumbe wote wa mkutano
mkuu, lakini makada wenzake wamekuwa kimya, hawajalalamikia kitendo
chake hicho.
RAIS Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha kutumia
nguvu kupita kiasi kwa wananchi wakati linapotekeleza majukumu yake ya
kazi.
Pia amelitaka kuwa makini kutokana na nchi kukabiliwa na mambo matatu
muhimu ya uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapigakura, kura ya maoni ya
Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu.
Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipofunga mafunzo ya
uongozi katika ngazi ya urakibu katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi
Kurasini (DPA).
Alisema polisi wanayo haki ya kuwachukulia hatua wananchi wanapodai haki lakini wafuate utaratibu ili wasivunje amani.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwaonya wananchi kutokujichukulia sheria
mkononi akisema jeshi la polisi halitawafumbia macho watakaovunja
sheria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Anne Kilango
MWONGOZO wa ada elekezi utakaondoa utata wa utofauti wa kulipa ada
baina vyuo na vyuo nchini, unatarajiwa kukamilika na kuanza rasmi
kutumika mwezi ujao.
Kwa sasa mwongozo huo umeshaandaliwa na kinachosubiriwa ni mfumo wa
kompyuta utakaosaidia kukokotolea ada zitakazotumika katika vyuo vikuu
nchini ambao ndio utakamilika rasmi Aprili mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Anne Kilango, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina
Makilagi (CCM), aliyetaka kujua mchanganuo wa ada baina ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na endapo
unaendana na hali halisi.
Akijibu swali hilo, Kilango alikiri kuwa kumekuwa na tatizo hilo la
utofauti wa utozaji ada katika vyuo mbalimbali nchini kwa muda mrefu, na
kwa sasa Tanzania ina vyuo vikuu 53 na taasisi 21 zinazotoa shahada. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Waziri mkuu wa Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei. David
Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya tatu inaweza kuwa ni
kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni vizuri
kuchaguliwa.
Chama kikuu cha upinzani cha Leba kimemshutumu Bwana
Cameron kwa kuonyesha uzembe na kushinikiza muhula wa tatu, kwa chama
chake cha Conservative, hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mabeki wa Coastal Union wakiwahani mpira na wachezaji waAzam wakati
wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa
Mkwakwani ,Tangajuzi.Azam ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu
amesema walihitaji ushindi wa zaidi ya bao moja dhidi ya Coastal Union
ila walikwamishwa na uwanja mbovu wa Mkwakwani na kushindwa kuonyesha
kiwango chao cha juu.
Mechi hiyo iliyochezwa juzi ilimalizika kwa
ushindi wa bao 1-0 kwa Azam na kuendelea kukaa katika nafasi ya pili
kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya pointi moja
dhidi ya Yanga wenye 37.
Bao pekee la Azam lilifungwa na mshambuliaji wao,
John Bocco, na Kavumbagu alilazimika kutolewa nje huku nafasi yake
ikichukuliwa na Gaudence Mwaikimba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
amewataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanafunga mabao mengi na
kutoruhusu bao katika kila mechi watakayocheza kama wana nia ya
kuipokonya ubingwa Azam FC.
Cannavaro alisema katika kipindi hiki ambacho
Yanga na Azam FC zinaeendelea kushindana kileleni mwa msimamo wa Ligi
Kuu kitu pekee kinachotakiwa ni kufunga mabao mengi ili mwisho tofauti
ya mabao inaweza kuamua bingwa.
Cannavaro alisema kwa hatua ambayo ligi imefikia
ni lazima kila mchezaji apambane kuhakikisha timu inamaliza ikiwa bingwa
na si vinginevyo kwani malengo yao msimu huu yalikuwa ni kutwaa taji.
“Inapotokea nafasi ya kufunga tunatakiwa tufunge
pasipo kuangalia kuwa mfungaji ni beki, kiungo au mshambuliaji. Pia
wakati wa kujilinda inatakiwa kila mchezaji ashiriki kuzuia na kulinda
magoli, hapo tunaweza kuwa mabingwa bila wasiwasi.
Njia nzuri zaidi ya kuonyesha hilo ni angalau kufunga mabao mawili kwenye kila mechi mpaka mwisho wa msimu,” alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema ushindi walioupata dhidi ya
Mgambo JKT juzi Jumapili, umerudisha morali ya kikosi chao kuelekea
mechi za mwishoni mwa ligi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Michuano
ya netball ya Afrika ya Mashariki imemalizika Zanzibar huku timu ya
MOICT ya Kenya ikitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake baada ya kuifunga
timu ya NIC ya Uganda kwa mabao 32-29.
NIC ndio walikuwa mabingwa
watetezi baada ya kulinyakua kombe hilo mwaka jana katika michuano
iliyofanyika Dar es Salaam. Hii ni mara ya pili kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuandaa michuano hiyo mara mbili mfululizo, zamu hii ikiwa
ni upande wa Tanzania Zanzibar (visiwani) katika viwanja vya Gymkhana.
Netball,
au mpira wa pete ni mchezo ambao kwa miaka mingi umekuwa ukihusisha
timu za wanawake pekee, lakini katika kuleta usawa (gender balance) kama
ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa kikapu (basketball), wavu
na mingineyo, mchezo huo katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa
ukishirikisha timu za wanaume katika kuleta hamasa na ushindani.
Kwa
upande wa wanaume, wenyeji Polisi ya Zanzibar waliibuka washindi wa
michuano hiyo ya Afrika Mashariki, baada ya kuwafunga wenzao wa JKU (pia
ya Zanzibar) kwa mabao 38-34 katika mechi ya vuta nikuvute.
Michuano
hiyo hufanyika kila mwaka kwa nchi wanachama kupeana zamu za kuandaa
mashindano hayo. Nchi zilizoshiriki ni wenyeji Zanzibar, Kenya, Uganda
na Tanzania Bara.
Rwanda na Burundi ni sehemu ya jumuiya hiyo ya Afrika
ya Mashariki lakini hawana historia kubwa ya kuwa sehemu ya kuwa nchi
shiriki. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Baadhi ya wachezaji wa kiafrika watakaathirika na sheria hiyo.
Shirikisho
la kanda kanda nchini England FA sasa linakusudia kuandaa sheria
itakayo kupunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa
Ulaya watakaosajiliwa katika ligi za nchi hiyo.
Mwenyekiti wa
shirikisho hilo Greg Dyke asema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye
hatari ya kutowasaidia wachezaji raia wa Uingereza kama hatua
hazitachukuliwa.
Katika mpango pia itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji waliokulia nchini humo.
Mikakati hiyo yote ni ya kuimarisha timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za kimataifa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KAMATI maalumu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), imekamilisha kazi
ya ugawaji wa majimbo 211 ambayo ni sawa na asilimia 88 kati ya majimbo
yote 239, imefahamika.
Wakati hayo yakiendelea, kamati hiyo imeshindwa kuafikiana katika
majimbo 28 ambayo yanasubiri uamuzi wa wenyeviti wa vyama vinavyounda
Ukawa, ambao watamaliza kiporo hicho mwezi huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa juu wa umoja huo, kutangaza
mkakati wa kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo ya
uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba. Ukawa ni umoja ulioanzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu
la Katiba, ukiundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kamati hiyo maalumu ya Ukawa,
kiliiambia MTANZANIA jana kuwa kwa muda wa wiki moja sasa, kamati hiyo
imekamilisha kazi hiyo kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeelezwa
linaweza kutoa upinzani mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika
Uchaguzi Mkuu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa na wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni.
RAIS
Jakaya Kikwete ameziagiza mamlaka za ulinzi na usalama kuhakikisha
shughuli ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, upigaji kura ya
Katiba Inayopendekezwa unafanyika kwa amani na wasioitakia mema nchi
wasibadilishe matukio hayo kuwa fujo na kuingiza nchi kwenye vurugu.
Alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua mafunzo elekezi kwa wakuu
wapya 27 wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni huku akiwataka kuwa na
ushirikiano na vyama vyote vya siasa.
Alisema kazi ya kuboresha daftari la wapiga kura, imeanzia Njombe na
itaendelea mikoa mingine na kuwataka viongozi hao kuhamasisha wananchi
kujitokeza kwa wingi na kukumbusha maana ya kuwa na kitambulisho cha
kura ambacho kitamwezesha kupiga kura ya maoni na katika uchaguzi mkuu
mwaka huu.
“Wananchi wasipoteze fursa waone haja ya kujiandikisha na watakaokosa
fursa ya kupiga kura hawataipata fursa hiyo tena. Tunataka Watanzania
wenye sifa washiriki kikamilifu kuhimiza wananchi wajiandikishe, na
kupiga kura,” alisema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WAKATI
wadau wa usafiri nchini wakipendekeza kushuka kwa nauli za daladala na
mabasi yaendayo mikoani, wamiliki wa mabasi wametishia kufuta utaratibu
wa kutowatoza nauli askari na kuongeza kuwa, hata nauli pungufu za
wanafunzi sasa zitakuwa historia.
Wadau wamependekeza kupunguzwa kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani
kwa viwango vya kati ya asilimia 15 na 25 huku wakitaka nauli za
daladala zipungue kutoka Sh 400 hadi Sh 300 kwa njia ya umbali wa
kilometa 10.
Hayo yaliibuka jana wakati wa mkutano wa wadau kukusanya maoni kuhusu
mapitio ya viwango vya nauli za mabasi ya mikoani na daladala kupungua
kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta ulioandaliwa na Mamlaka ya
Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra). Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.