Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Anne Kilango
MWONGOZO wa ada elekezi utakaondoa utata wa utofauti wa kulipa ada
baina vyuo na vyuo nchini, unatarajiwa kukamilika na kuanza rasmi
kutumika mwezi ujao.
Kwa sasa mwongozo huo umeshaandaliwa na kinachosubiriwa ni mfumo wa
kompyuta utakaosaidia kukokotolea ada zitakazotumika katika vyuo vikuu
nchini ambao ndio utakamilika rasmi Aprili mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Anne Kilango, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina
Makilagi (CCM), aliyetaka kujua mchanganuo wa ada baina ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na endapo
unaendana na hali halisi.
Akijibu swali hilo, Kilango alikiri kuwa kumekuwa na tatizo hilo la
utofauti wa utozaji ada katika vyuo mbalimbali nchini kwa muda mrefu, na
kwa sasa Tanzania ina vyuo vikuu 53 na taasisi 21 zinazotoa shahada. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Alisema ada katika vyuo vikuu vya umma ikiwa ni pamoja na UDSM na
UDOM, zinatofautiana kati ya chuo na programu wanayosomea wanafunzi.
Alisema, mfano programu ya uhandisi UDSM ada yake ni Sh milioni 1.3
wakati UDOM programu hiyo ni Sh milioni 1.5 na katika programu za
Sayansi na Ualimu UDSM inatoza ada Sh milioni 1.3 wakati UDOM unatoza Sh
milioni 1.2.
Alisema kwa kuzingatia tofauti za kiasi cha ada kinachotozwa na vyuo
vikuu nchini, Serikali ilifanya utafiti wa kina kwa kushirikisha wadau
mbalimbali ili kuweza kupanga ada elekezi kwa programu zote
zinazofundisha katika vyuo vyote vikuu.
“Mwongozo wa ada elekezi umekwishaandaliwa na kwa sasa Serikali
inaandaa mfumo wa software wa kukokotoa ada zitakazotumika katika vyuo
vikuu vyote nchini,” alisema.
Akijibu swali la nyongeza la Makilagi aliyekata kujua Serikali ina
mkakati gani wa kuingiza shule binafsi katika mpango huo, Kilango
alisema Serikali inatoa maelekezo ya ada kwa vyuo vya serikali kwa kuwa
vyenyewe vinalipwa ruzuku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment