Michuano
ya netball ya Afrika ya Mashariki imemalizika Zanzibar huku timu ya
MOICT ya Kenya ikitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake baada ya kuifunga
timu ya NIC ya Uganda kwa mabao 32-29.
NIC ndio walikuwa mabingwa
watetezi baada ya kulinyakua kombe hilo mwaka jana katika michuano
iliyofanyika Dar es Salaam. Hii ni mara ya pili kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuandaa michuano hiyo mara mbili mfululizo, zamu hii ikiwa
ni upande wa Tanzania Zanzibar (visiwani) katika viwanja vya Gymkhana.
Netball,
au mpira wa pete ni mchezo ambao kwa miaka mingi umekuwa ukihusisha
timu za wanawake pekee, lakini katika kuleta usawa (gender balance) kama
ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa kikapu (basketball), wavu
na mingineyo, mchezo huo katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa
ukishirikisha timu za wanaume katika kuleta hamasa na ushindani.
Kwa
upande wa wanaume, wenyeji Polisi ya Zanzibar waliibuka washindi wa
michuano hiyo ya Afrika Mashariki, baada ya kuwafunga wenzao wa JKU (pia
ya Zanzibar) kwa mabao 38-34 katika mechi ya vuta nikuvute.
Michuano
hiyo hufanyika kila mwaka kwa nchi wanachama kupeana zamu za kuandaa
mashindano hayo. Nchi zilizoshiriki ni wenyeji Zanzibar, Kenya, Uganda
na Tanzania Bara.
Rwanda na Burundi ni sehemu ya jumuiya hiyo ya Afrika
ya Mashariki lakini hawana historia kubwa ya kuwa sehemu ya kuwa nchi
shiriki. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment