Tuesday, March 24, 2015

CANNAVARO ATAKA MABAO MENGI YANGA

 Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro
 
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanafunga mabao mengi na kutoruhusu bao katika kila mechi watakayocheza kama wana nia ya kuipokonya ubingwa Azam FC.
Cannavaro alisema katika kipindi hiki ambacho Yanga na Azam FC zinaeendelea kushindana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kitu pekee kinachotakiwa ni kufunga mabao mengi ili mwisho tofauti ya mabao inaweza kuamua bingwa.
Cannavaro alisema kwa hatua ambayo ligi imefikia ni lazima kila mchezaji apambane kuhakikisha timu inamaliza ikiwa bingwa na si vinginevyo kwani malengo yao msimu huu yalikuwa ni kutwaa taji.
“Inapotokea nafasi ya kufunga tunatakiwa tufunge pasipo kuangalia kuwa mfungaji ni beki, kiungo au mshambuliaji. Pia wakati wa kujilinda inatakiwa kila mchezaji ashiriki kuzuia na kulinda magoli, hapo tunaweza kuwa mabingwa bila wasiwasi.
Njia nzuri zaidi ya kuonyesha hilo ni angalau kufunga mabao mawili kwenye kila mechi mpaka mwisho wa msimu,” alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema ushindi walioupata dhidi ya Mgambo JKT juzi Jumapili, umerudisha morali ya kikosi chao kuelekea mechi za mwishoni mwa ligi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...