Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu
amesema walihitaji ushindi wa zaidi ya bao moja dhidi ya Coastal Union
ila walikwamishwa na uwanja mbovu wa Mkwakwani na kushindwa kuonyesha
kiwango chao cha juu.
Mechi hiyo iliyochezwa juzi ilimalizika kwa
ushindi wa bao 1-0 kwa Azam na kuendelea kukaa katika nafasi ya pili
kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya pointi moja
dhidi ya Yanga wenye 37.
Bao pekee la Azam lilifungwa na mshambuliaji wao,
John Bocco, na Kavumbagu alilazimika kutolewa nje huku nafasi yake
ikichukuliwa na Gaudence Mwaikimba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kavumbagu aliliambia gazeti hili kuwa anaamini
bado ana nafasi ya kufunga zaidi katika mechi zilizobaki lakini kwa sasa
anaangalia zaidi ushindi wa timu ili iweze kutetea ubingwa, hivyo
mchezaji yeyote atakayeifungia Azam hataweza kuharibu mahesabu yake.
“Hii mechi tungepata mabao mengi ila uwanja
umetukwamisha sana, nafurahi timu yangu imeshinda japo kwa ushindi wa
bao moja, naamini nitafunga mechi zijazo na ninafurahi mchezaji
mwenzangu anapoifungia Azam kwani wote tupo kwa ajili ya kufanikisha
tunatetea ubingwa,” alisema Kavumbagu.
Kavumbagu ameshafunga mabao kumi akifuatiwa na Simon Msuva wa Yanga ambaye amefikisha mabao tisa.
Kocha Msaidizi wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelu
‘Julio’ amesikitishwa na timu yake kufungwa na mabingwa watetezi, Azam
FC, kitendo ambacho kimewadhalilisha kwa kile alichodai kuwa wamefungwa
na timu mbovu.
Coastal Union ilifungwa bao 1-0 na Azam juzi kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani.
Julio alisema anashangazwa na mpira wa kiwango cha
chini unaochezwa na Azam, ambayo ina kila kitu kuanziamiundombinu na
kuwalipa fedha nzuri wachezaji ambao yeye alidai kuwa kiwango chao ni
cha chini na hawapaswi kuwa hapo.
“Kinachoniuma ni kufungwa na timu mbovu kama Azam,
nashindwa kuelewa wachezaji wa Azam wana matatizo gani hadi wanacheza
kwa kiwango cha chini kiasi hiki, Azam ina kila kitu tofauti na hizi
timu zetu na kwa mfumo huu sidhani kama wanaweza kufika mbali kisoka.
“Nafikiri hawana mipango mizuri katika usajili
ndiyo maana wachezaji waliopo wanashindwa kuipa hadhi klabu yao kwa
kuonyesha soka safi, tumefungwa ila wachezaji wangu wameonyesha kiwango
kizuri japokuwa nafasi walizozipata wameshindwa kuzitumia kama wenzetu
ambao wanabutua butua tu,” alisema Julio.
Kocha wa Azam, George Nsimbe alisema: “Kwa sasa
hatutaki kuangalia tunafunga mabao mangapi, kikubwa tunachopigania ni
kupata pointi tatu kila mechi na hii ni kutokana kwamba tuna lengo la
kutetea ubingwa, mechi zilizobaki tunatakiwa kushinda zote. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment