Tuesday, March 24, 2015

KIKWETE AIONYA POLISI MATUMIZI YA NGUVU

jk
RAIS Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha kutumia nguvu kupita kiasi kwa wananchi wakati linapotekeleza majukumu yake ya kazi.

Pia amelitaka kuwa makini kutokana na nchi kukabiliwa na mambo matatu muhimu ya uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapigakura, kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipofunga mafunzo ya uongozi katika ngazi ya urakibu katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Kurasini (DPA).
Alisema polisi wanayo haki ya kuwachukulia hatua wananchi wanapodai haki lakini wafuate utaratibu ili wasivunje amani.

Hata hivyo, Rais Kikwete aliwaonya wananchi kutokujichukulia sheria mkononi akisema jeshi la polisi halitawafumbia macho watakaovunja sheria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
 “Hatuwezi kushurutishwa kwa vurugu na mabomu, utaratibu huu hauwezi kulisaidia jeshi la polisi.
“Tanzania inasifiwa kuwa ni kisiwa cha amani hivyo polisi wajitahidi kulinda raia na mali zao kwa kufanya kazi kwa weledi. Dumisheni kazi njema na kuboresha amani nchini,”alisema rais Kikwete.

Aliwataka polisi kuwa makini na kujiandaa kukabiliana na shughuli muhimu za upigaji kura ya maoni, uandikishaji daftari la kupiga kura na uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Alisema ni muhimu wawe makini kuhakikisha nchi inavuka salama katika mambo hayo matatu mazito.

Serikali itahakikisha inatoa vitendea kazi kwa wakati ili vianze majaribio kabla ya siku ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, alisema.

Rais pia alizungumzia suala la ugaidi akisema kutokana na mambo hayo mitatu kuna dalili za watu kujiandaa kufanya matukio ya ugaidi kutokana na viashiria vilivyoanza kujitokeza.

Kuhusu uuzaji na usafirishaji dawa za kulevya, Rais Kikwete alisema katika kesi za hizo, watu 935 walikamatwa wakiwamo vigogo 19 ambao kesi zao zipo mahakamani.

Alisema waathirika wakubwa wa dawa za kulevya ni vijana hivyo tatizo hilo lisipokomeshwa mapema nchi itakuwa na vijana mazezeta. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na MTANZANIA

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...