Rais
Jakaya Kikwete akiwa na wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni.
RAIS
Jakaya Kikwete ameziagiza mamlaka za ulinzi na usalama kuhakikisha
shughuli ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, upigaji kura ya
Katiba Inayopendekezwa unafanyika kwa amani na wasioitakia mema nchi
wasibadilishe matukio hayo kuwa fujo na kuingiza nchi kwenye vurugu.
Alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua mafunzo elekezi kwa wakuu
wapya 27 wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni huku akiwataka kuwa na
ushirikiano na vyama vyote vya siasa.
Alisema kazi ya kuboresha daftari la wapiga kura, imeanzia Njombe na
itaendelea mikoa mingine na kuwataka viongozi hao kuhamasisha wananchi
kujitokeza kwa wingi na kukumbusha maana ya kuwa na kitambulisho cha
kura ambacho kitamwezesha kupiga kura ya maoni na katika uchaguzi mkuu
mwaka huu.
“Wananchi wasipoteze fursa waone haja ya kujiandikisha na watakaokosa
fursa ya kupiga kura hawataipata fursa hiyo tena. Tunataka Watanzania
wenye sifa washiriki kikamilifu kuhimiza wananchi wajiandikishe, na
kupiga kura,” alisema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Pia alisema kuna zoezi la kutoa elimu, kampeni kabla ya kura ya
maoni, kutumia vizuri mamlaka ya ulinzi na amani ili mazoezi hayo
yafanyike kwa amani na utulivu.
“Wasioitakia mema nchi hii wasifanye zoezi hili likageuka la fujo na
kuhujumu kampeni, wahakikishe mazoezi hayo yanafanikiwa,” alisema. Pia
Rais Kikwete alisema mwaka huu unafanyika uchaguzi mkuu akiwa ametimiza
haki yake ya kikatiba.
“Nimetimiza fursa yangu ya kikatiba, baada ya
uchaguzi wa Oktoba ninakuwa mzee maarufu, tufanye uchaguzi kwa utulivu
na amani ili Watanzania wapate nafasi ya kuchagua kiongozi anayefaa,”
alisema.
Alisema kuna matatizo makubwa ya mauaji ya walemavu wa ngozi na
usafirishaji wa dawa za kulevya, masuala ambayo yanalitia fedheha taifa.
“Ni jambo la aibu, kijinga na fedhehesha mtu mzima na akili yako
unaamini ukipata kidole cha albino mambo yako yatakuwa mazuri, kamati za
ulinzi na usalama zikae na kuona namna gani watakabiliana na suala kama
hili,” alisema.
“Lipo tatizo kubwa la dawa za kulevya ambapo vijana wanavuruga sifa
nzuri ya Taifa, sasa mtu akienda nje ya nchi akijitambulisha anatoka
Tanzania anaonekana anasafirisha dawa za kulevya. “Kiwango cha ukubwa
kinatofautiana, kila mahali tatizo hili ni kubwa sana zinatakiwa juhudi
zaidi, lakini ni tatizo kubwa,” alisema.
Uteuzi wa wakuu wa wilaya Rais Kikwete alisema wakuu wa wilaya wapya waliteuliwa kutokana na kukidhi sifa na vigezo. Pia aliwaonya wakuu wa wilaya wanaotumia madaraka yao vibaya kwa
kukamata wananchi na kuwaweka ndani bila sababu za msingi, kwani baadhi
yao wanajiona wana madaraka zaidi kuliko Rais wa nchi.
Alisema wakuu wa wilaya waliteuliwa kutokana na kukidhi sifa na
vigezo vya madaraka yao na kuwataka wakachape kazi ili wakidhi matarajio
aliyokuwa nayo na kuwataka kutokaa maofisini kwani wanafanya kazi na
jamii wanatakiwa kujua shida za watu.
“Nimewaamini naomba mkafanye kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa,”
alisema. Aliwataka kurejea vituo vyao vya kazi na kutekeleza kwa ufanisi
mkubwa kazi zao kwa kipindi kifupi kilichobaki kabla ya kuingia
uchaguzi mkuu.
“Mkuu wa wilaya ndiye mwakilishi wa Rais, zamani watu walikuwa na
msemo wa kula nchi kwani wanasema hapa Rais amenikatia kipande changu
sasa sio kula nchi bali kujenga nchi,” alifafanua.
Akizungumzia ujenzi wa maabara alisema kuna wilaya zimekamilisha
ujenzi, lakini aliongeza miezi sita inaisha Juni kila mmoja ajue ujenzi
umefikia hatua gani na kusimamia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment