Wajumbe
wa mashirika ya kiraia wa vijiji vya Tama na Itala kusini mwa tarafa la
Lubero jimboni kivu kaskazini, wanasema kutishiwa na kundi la waasi wa
kihutu toka Rwanda wa FDLR kundi wanao ongozwa na Kanali Kizito.
Vitisho
hivyo vinakuja kutoka uchapishaji wa ripoti wa mashirika ya kiraia
katika sekta hio inayo bainisha hali ya harakati makundi ya waasi na
wanamgambo katika maeneo hayo ambao wanahusika naunyanyasaji dhidi ya
raia.
Baadhi ya wanachama wa vyama vya kiraia katika vijiji vya
Tama na Itala wanasema kua raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali
ya mafichoni kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi
wanao hishi maeneo hayo hasa FDLR huku wakisema nawaishi kwa tabu
wakilala usiku misituni. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Vitisho hivyo pia vinasababisha umati wa
wakazi wamiji ya Kalevia, Bunyangenge, Bukumbirwa, Misingi, Mbwambali na
Ikobo kuyaama makaazi yao nakuamia katika maeneo salama yanayo
dhibitiwa na jeshi la taifa.
Mashirika ya kiraia wanaomba serekali
kuanzisha operesheni zakijeshi dhidi ya waasi wa FDLR kuanzishwa pia
kusini mwa Lubero ambako operesheni za kijeshi zimeanzishwa wiki chache
dhidi ya waasi wakihutu toka Rwanda wa FDLR katika jimbo la Kivu
Kaskazini.
Baadhi ya vyanzo katika kanda hio zinaonyesha kuwa
kiongozi wa waasi hao wa FDLR kanali Kizito wkundi maarufu la
Foca,aliwateka nyara wanakijiji wa Mukeberwa na sehemu ya mji wa Kiyamba
ilioko kusini mwa Tarafa la Lubero. Hata hviyo kiongozi huyo wa
wanamgambo hao wa FDLR huwakataza wakaazi kuto toka ao kuingia ndani ya
vijiji vyao.
Niwiki tatu sasa toka jeshi la hapa nchini FARDC
kuanzisha harakati za kijeshi katika mkoa wa kivu kusini na kivu
kaskazini ilikuwapokonya silaha waasi hao wakihuto kutoka rwanda wa FDLR
,harakati zinazoendeshwa mashambulizihayo na jeshi la Kongo peke yao
baada ya serikali ya Congo kukataa msaada toka vikosi vya umoja wa
matifa MONUSCO. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment