BAADA ya miezi mitano ya mazungumzo ya kurejesha amani Sudan Kusini
yaliyoratibiwa na chama tawala, CCM, hatimaye Rais wa nchi hiyo, Salva
Kiir na hasimu wake, Riek Machar wamesaini makubaliano ya kusitisha
mapigano, yaliyoibuka tangu mwaka 2011.
Kutokana na machafuko hayo, zaidi ya raia 20,000 wa Sudan Kusini,
wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni moja wakikosa makazi.
Walisaini makubaliano hayo juzi usiku jijini hapa, huku marais wa
ndani na nje ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, wakishuhudia.
Wengine walioshuhudia makubaliano hayo ni Rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta, Naibu Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa , Rais wa
Uganda, Yoweri Museveni, Salva Kiir, Riek Machar na Makamu wa Rais wa
Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.