Mtandao
wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hiyo kupitia
programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.
WhatsApp
ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa imechukua hatua dhidi ya
watumiaji wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya wasiwasi kwamba
programu hiiyo huenda iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za
watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio bandia na isio rasmi ya Android inawezesha watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu
wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa kuwa makini na
kutahadhari kuhusu wanavyodownload programu flani au 'Apps'. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mtandao
wa WhatsApp ulisema hivi karibuni kwamba ina watumiaji milioni 700
wanaotuma ujumbe bilioni 30 kila siku. Kwa sasa inatoza dola 0.99 kwa
watumiaji wake wanaotumia huduma ya WhatsApp Plus kila mwaka.
''Lengo
letu ni kuhakikisha kwamba huduma ya WhatsApp ni ya kasi kwa
wanaoitumia, hilo ndio jambo muhimu sana kwetu,'' alisema msemaji wa
kampuni hio.
''Watu wengine wamebuni progarmu ambazo bado
hazijaidhinishwa na sasa wanazitumia na WhatsApp , kitu ambacho kinaweza
kusababisha kupotea kwa ujumbe au baadhi ya taarifa kuvujishwa. ''
''Bila
shaka jambo hili linakwenda kinyume na malengo yetu ya kutoa huduma kwa
wateja wetu. Kuanzia leo tutaanza kuchukua hatua kali dhidi ya
wanaotumia programu ambazo hazijaithinishwa ili kuweza kutumia programu
zetu na pia kuwatahadharisha wanaozitumia programu hizo''.
Kulingana
na moja ya maduka ya kuuza programu za kwenye mitandao, programu ya
WhatsApp Plus yenyewe ilikuwa imekuwa dowloaded mara milioni 35. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment