Friday, January 23, 2015

TETESI ZA USAJILI: DE GEA KUUZWA?

 De Gea
Mustakabali wa kipa David de Gea kusalia Manchester United upo shakani baada ya wakala wake Jorge Mendes kushindwa kuwakatalia Real Madrid mpango wa kumsajili.
Manchester United inajianda kutoa ofa kwa timu ya Villarreal ili kumpata kumpata beki Gabriel Paulista, raia wa Brazil ambae yuko kwenye mazungumzo na Arsenal.
Klabu ya Chelsea iko katika mipango ya kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa.
Bosi wa West Brom Tony Pulis imethibitisha kuhitaji kuwasajili winga wa Wigan Callum McManaman na kiungo Darren Fletcher toka Man United katika dirisha hili la usajili.
Timu ya QPR imetoa ofa ya kumsajili mshambuliji wa zamani Ac Milan Alexandre Pato,anayechezea timu ya Sao paul kwa mkopo.
Meneja wa Swansea City Garry Monk anavutiwa na mpango wa kumsajilibeki wa kushoto wa Norwich Martin Olsson, mwenye miaka 26,pamoja na kiungo Alexandru Maxim toka Stuttgart
Kipa wa Manchester United David da Gea
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia winga wake Raheem Sterling, atasaini mkataba wa muda mrefu kusalia klabu hapo siku chache zijazo. Manchester City wameulizia uwezekano wa kumpata mshambuliaji Jay Rodriguez wa timu ya Southampton.
Hull City wanamfuatilia winga wa Tottenham timu Taifa ya England Aaron Lennon,ambae anataka kuondoka White Hart Lane kwa kukosa namba kikosi cha kwanza.
Kiungo wa zamani wa Chelsea Kevin de Bruyne,amekata kurejea katika ligi ya England kwa kusema havutiwi kurudi katika ligi pamoja na kwepo taarifa za kuwaniwa na Arsenal na Manchester United.
Klabu ya Roma inajaribu kiwashawishi Chelsea kukubali pauni 380,000 ili kumchukua winga Mohamed Salah kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...