Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya
Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba
Yahya
KATIKA kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa hususan kuwatafutia ajira Watanzania nje ya
nchi, Wizara hiyo kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, Umoja
wa Falme za Kiarabu umefanikisha kulishawishi Shirika la Ndege la
Emirates kuajiri Watanzania wengi zaidi kuanzia mwaka 2015.
Emirates, moja ya mashirika ya ndege tajiri zaidi duniani, linamiliki
zaidi ya ndege za kisasa 280, huku likiwa na safari za uhakika duniani
kote.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya
Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba
Yahya alisema shirika hilo litaajiri Watanzania katika kada mbalimbali.
“Wamekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo maofisa
wake wanaosimamia ajira watakuja nchini (Tanzania) Machi 2015 kwa ajili
ya kuwafanyia usaili Watanzania watakaoomba kazi hizo na kupata uteuzi
wa awali,” alisema.
Aliwataka Watanzania kuchangamkia ajira hizo, ambazo awali
zilitangazwa Julai 2014, lakini ni Watanzania wachache tu walioomba na
hivyo kutofikia lengo lililokusudiwa.
“Baada ya mazungumzo ya kina, uongozi wa Emirates umekubali kuongeza
muda wa kuzitangaza ajira hizo kwa mara nyingine na kupanga kufanya
usaili kama ilivyoelekezwa hapo awali,” alisema.
Aliwasisitiza Watanzania wenye sifa na vigezo stahiki, kutumia fursa
hiyo kuomba nafasi hizo na pia kujiandaa vyema katika usaili ili
wajihakikishe ajira katika soko la ajira la kimataifa.
Kaimu Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania
(TaESA), Boniface Chandaruba aliwataka waombaji wote kuhakikisha
wanapata barua kutoka wakala huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment