Saturday, April 27, 2013

MGANGA AELEZEA ISHU YA DIAMOND KUNG'ANG'ANIA MAITI YA BI.KIDUDE KWA NIA YA KUIBA NYOTA YAKE

Baada ya msiba wa Bi Kidude kumalizika, hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ alibaki peke yake na mwili wa marehemu chumbani kwa ajili ya kuchota nyota ya Bi. Kidude.
Leo tunaye Dr Salum Mkumba ambaye ataeleza kwa kirefu tafsiri ya kitendo alichokifanya Diamond.
Funguka: Dr Mkumba asalam aleikum, karibu ndani ya nyumba kubwa ya magazeti Pendwa Tanzania, Global Publishers Ltd.
Dr Mkumba: Waaleikum salaam, ahsanteni nashukuru. Mimi leo nina jambo ninataka niliweke sawa.
Funguka: Liweke sawa, sisi pamoja na wasomaji wetu wa Risasi Jumamosi tunakusikiliza.
Dr Mkumba: Nataka kuweka sawa juu ya suala la nyota, mtu akifariki huwa anakwenda na nyota yake sasa nimeshangaa kusikia Diamond alikwenda kuchukua nyota ya marehemu.
Funguka: Sasa Diamond alipobaki peke yake chumbani na mwili wa marehemu ilikuwa ina maana gani?
Dr Mkumba: Pale alikuwa anajaribu kujisafisha tu katika jamii, hakuna cha ziada.
Funguka: Unaposema anajisafisha, kwani amechafuka?
Dr Mkumba: Eee! Kwani hujui? Amenaswa na mke wa mtu hotelini, skendo za wanawake tofauti zimekuwa zikimtafuna kila kukicha.
Funguka: Unaposema alikuwa anajisafisha una kitu gani cha kushika mkononi?
Dr Mkumba: Surat Nnajimi Sura ya 39 imezungumza kwa kirefu ila tafsiri yake ipo hivi; hakuna anachokichuma mwanadamu kwa marehemu ila marehemu anategemea kuombewa dua na mtu mzima.
Funguka: Kwa hiyo ina maana vile alivyofanya Diamond ni kazi bure?
Dr Mkumba: Nakwambia hakuna cha maana zaidi ya kujisafisha.
Funguka: Sasa una mshauri nini Diamond?
Dr Mkumba: Amrudie mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada ya kweli.
Funguka: Vipi kuhusu suala la kujenga msikiti ambalo Diamond alitangaza kuwa ana mpango huo?
Dr Mkumba: Hapo ndiyo kabisa, ajenge tu lakini haisaidii kitu sababu ukijenga nyumba ya ibada inatakiwa utumie fedha ambazo umezipata kihalali katika njia safi.
Funguka: Kwani fedha zake hajazichuma kwa njia safi?
Dr Mkumba: Kiimani yetu ya Kiislam muziki siyo halali hivyo fedha anayoipata kwenye muziki haiwezi kuwa halali.
Funguka: Tunashukuru, karibu tena siku nyingine.
Dr Mkumba: Haya Ishallah!

FATAKI LANASWA LIVE NA MWANAFUNZI GESTI WAKIWA UCHI WA MNYAMA WAKILA URODA..!!



MfanyabiAshara ‘alwatani’ Bongo, mkazi wa jijini Dar, Allain Tajiri amekumbwa na skendo nzito baada ya kufumaniwa na mwanafunzi wa sekondari wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu katika chumba namba 107 kwenye gesti iitwayo Jamboz iliyopo Kinondoni jijini Dar.

Habari za uhakika zilieleza kuwa tukio hilo lilikuwa ni mtego baada ya walezi wa denti huyo kunasa mawasiliano ya mfanyabiashara huyo akimrubuni binti yao.


Katika mawasiliano hayo, Tajiri alimtaka denti huyo wa sekondari moja iliyopo Kibamba, Dar (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum za weledi wa uandishi wa habari), wakutane kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kuimomonyoa amri ya sita.

Baada ya walezi hao kuufuma ujumbe kwenye simu ya binti yao, walimuwekea doria bila mwenyewe kujijua na ulipokaribia muda waliokubaliana kukutana gesti, denti huyo aliaga anakwenda ‘tuisheni’.

AIBU ! KIJANA ANASWA AKIMNAJISI NA KUMLAWITI MBUZI HADHARANI....!!

Katika  hali  ya  kushangaza, jamaa  mmoja  nchini  Nigeria  amenaswa  live  akivunja  amri  ya  sita  na  Mbuzi ....
Baada  ya  kufamaniwa  na  wanachi, mwanaume  huyo  alipewa  kichapo  kikali  na  kufangashwa  na  mbuzi  huyo  hadi kituo  cha  polisi.... 
Maswali  yenye  utata  kuhusu  tukio  hilo:
1. Kuna  faida  gani  au  starehe  gani  ya  kufanya  mapenzi  na  mnnyama....
2..Viungo  vya  mwanaume  ni  vikubwa  sana  ukilinganisha  na  vile  vya  mbuzi...huyu  jamaa  aliwezaje....Bora  angechukua  punda  kuliko   kumuonea  mbuzi  wa  watu..!!! 
Niimani  yetu  kwamba sheria  itamfundisha  adabu

KAULI YA MKE WA MBUNGE GODBLESS LEMA SASA HIVI KUHUSU LEMA KUSHIKILIWA POLISI

Taarifa za sasa kutoka Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.

Namkariri Mke wa Lema akiongea na TheTZA millardayo.com akisema “jana usiku saa sita kasoro watu walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka kuitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia gari mbona chochote hakikutokea?”

ISHA MASHAUZI ATIWA MBARONI KWA WIZI WA SH. 700, 000...!!

MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo ‘Mashauzi’, Jumatano iliyopita alikumbwa na masaibu mazito kufuatia kudakwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi, Dar akituhumiwa kukwapua mkoba wenye kitita cha shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya Veronica Tarik.
Chanzo cha habari kituoni hapo kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja Mtaa wa Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake.

Veronica aliwakimbiza wawili hao na kuwadaka mtaa wa pili na kuwasomea tuhuma zao kisha akawaomba awasachi kwenye mafurushi waliyobeba lakini Isha na mshirika wake waligoma, hali iliyosababisha kuzuka kwa timbwili wakidai mwanamke huyo alitaka kuwadhalilisha.

Baada ya Veronica aliyekuwa na wapambe ‘legelege’ kuzidiwa nguvu, waligeuka na kukimbilia Kituo cha Polisi Msimbazi ambako alifungua kesi ya wizi kwa Isha na shosti wake kwa jalada namba MS/RB/4023/2013.

MAGAZETI YA LEO APRIL 27, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.

DIAMOND ATANGAZA KUGAWA URODA KWA WAREMBO WA LONDON......!!

 
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’.
  

Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke.

Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.”

Friday, April 26, 2013

Lema kufikishwa Mahakamani juma tatu

 Lema akiongozana na wanafunzi wa chuo cha uhasibu baada ya wanafunzi hao kumpokea juzi chuoni hapo
Arusha,Tanzania

MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.
Mwanadishi wa Habarimpya.com mjini Arusha anasema kwamba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa ArushaLiberatus Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau.
"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili" alisema Sabas.
Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo. Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.
Mbunge huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.

WEMA AKODI NDENGE KUTOKA DAR KWENDA ARUSHA KWAAJILI YA MAPUMZIKO

 Habari Habari za uhakika zilieleza kuwa Wema na timu ya wafanyakazi katika kampuni yake ya Endless Fame Production, alikodisha ndege ya kifahari kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya mapumziko tangu Aprili 18 hadi 20, mwaka huu.

Ilifahamika kuwa ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na kampani yake tu.

CHANZO CHA YOTE NI DIAMOND

Ilibumburuka kuwa timu yake hiyo ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda kwenye mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.

Ilielezwa kuwa stresi alizokuwa nazo zilitokana na ile ishu ya kudaiwa kurekodiwa akibembeleza penzi kwa aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku mkali huku jamaa akiwa amelala na mpenziwe wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Baada ya kutokea kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza mawazo.
“Unajua ile ishu ilimchanganya sana bidada maana hakutegemea kama Diamond anaweza kufanya kitu kama kile so (kwa hiyo) alikwenda kutuliza akili na kweli sasa hivi walau yupo fresh (vizuri),” alisema sosi wa karibu wa Wema.
 
AINGIA ARUSHA KWA ULINZI MKALI
Walipoingia jijini Arusha, staa huyo wa Filamu ya The Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika hoteli ya bei mbaya aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege) hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo chetu,

PROFESA LIPUMBA AIPONDA CHADEMA NA KUDAI KUWA NI VINARA WA VURUGU NA HAWANA HOJA

Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya. 


“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.

HII NI BARUA YA WAZI KUTOKA MBEYA ILIYOANDIKWA KWA DIAMOND IKIMPONDA KWA MABAYA ANAYOYAFANYA.

BARUA KWA DIAMOND PLATINUMZ na MAMA YAKE MZAZI mbeya region P.O.BOX 1021 MBEYA 
dear diamond.... 
sina imani we ni mzima wa afya kutokana hasa na mambo unayofanya kiukweliii katika wasanii wakali mpaka kupitiliza hapa tz wew ni mmoja wapo.. napenda sana vibonzo vyako hasa kile cha " nani amenuna nani amenuna eti nani amenuna" najua utakua umemalizia WEMA... katika kila shoo zako unazofanyaga mara nyingi huwa unataja kumheshim sana mama yako mzazi kutokana na malezi aliyokupa toka kipindi kile unauza 
MITUMBA.. lakini saiz unafanya mama wa watu aonekane alizaa toto zinzi ambalo kama limetumwa kuzini na kuumiza wanaume wenzie.. ivi unajua mke anauma kias gani hata kama wanajileta we ni mtu mzima ambaye unatakiwa kupembua mambo.... hasa kuhusu jambo la HILI MBURULA LENZIO UWOZO or SORY I mean UWOYA.. unajua kabisa   kaka yetu NDIKU ambaye anafanya kazi ngumu ya kukabana na wakina NSAJIGWA NFUSO uwanjani ili apate chochte cha kulisha family yake lakini wew bila huruma una ramba asali yake... ivi unajua mtoto wa uwoya "krish" atakopukua njiani kwenda shule wenzie watakua daily wakimuambia " mtoto wa kambo wa DOMO huyo' ivi dear diamond mbna unataka mama yako asipewe heshma sababu ya wew hujui ka unamfanya awe despsd infrnt of da pple... najua hujaelewa coz elimu kwako ni tatizo utampigia wema akufafanulie ila usi mrecord coz anakusaidia ww.... au umea athirika unafanya kusambaza.. hawa wanawake wapo toka enzi za ma dinossaurs,,, mwambie penny akuambie maANA ya dinossaurs.. huu mda unaoangaika na wanawake ungejiendeleza ata kielimu iyo 4m four itakufksha wap.. na wew mama diamond ivi huoni anachofanya mwanao unashindwa kumshauli au unataka uje kumwambia akishaanza kuharisha na kumvisha visepe.. ERIC SHIGONGO naomba ukiiona hii itupie kwenye ijumaa wikienda ili babu yangu wa ileje Ambaye hatumiii fb asome mana kila siku amekua akiipenda nyimbo ya mbagala bila kujua uovu wa aliyeimba kwa leo yatosha ila TACAIDS naamini itakutemblea diamond siku si nyingi kkupa matumizi saHII YA arv

wako shabiki nambA MOJA DUNIA NZIMA....... via mbele kuchungu 
From:http://www.facebook.com/pachito.edd

WASANII WALIPONDA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA

BUNGE la Jamhuri la Muungano wa Tanzania limeonekana kuwachosha baadhi ya wasanii kutokana na kukosa hoja za maana za kujadili ndani ya bunge hilo na matokeo yake kuwa kama kijiwe kwa kutumia lugha chafu zilizokosa tija kwa taifa

Kutokana na hali hiyo ya baadhi ya wabunge kukosa lugha na sera zenye tija wawapo bungeni baadhi ya wasanii wanaliona hilo ni moja ya changamoto inayosababisha watanzania kuzidi kuwa na hari ngumu ya kimaisha kwa kukosa watetezi wenye umakini

Mmoja wa wasanii hao akizungumza na jarida hili Ben Pol alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wabunge kutumia lugha ya matusi  kwenye kujadili hoja na matokeo yake wanashindwa kupata muafaka wa wanayo yajadili

Alisema kuwa bunge limekosa muelekeo na ameacha kulisikiliza bunge hilo kwa sababu ya kukosa mueleko na kujaa lugha chafu za matusi huku wakishindwa kuyajadili yale ya msingi kwa taifa lao

Kutokana na hali hiyo nchi ya Tanzania itaendelea kubaki maskini na vitu kuendelea kupanda bei kila siku huku kipato cha wananchi kuwa duni kwa kukosa watetezi

Alisema kuwa bunge halijafika sehemu nzuri na kuonekana halina tija kwa wananchi wake na hali hiyo linasababisha wananchi kushindwa kupata ukombozi kwa yale wanayoyakusudiwa

Kwa upande wake msanii wa filamu nchini Rose Ndauka alisema kuwa bunge limekuwa si la wastaarabu na matokeo yake wanajadili vitu ambavyo havina tija kwa jamii

Alisema kuwa Tanzania ni nchini ya wastaarabu na wajadili vitu vya ustaarabu kwa kufikia muafaka hali hiyo imekuwa tofauti sasa kwa baadhi ya wabunge kujadili vitu kwa lugha chafu hali inayoshangaza taifa

"Wananchi tumewachagua wabunge huku tukiamini kuwa watafanya hilo tulilowaagiza ila hali imekuwa tofauti na mika mingine baadhi ya wabunge kuanza kujadili vitu visivyo na tija kwa wananchi wao" alisema Ndauka

LEMA ATUMIWA UJUMBE WA VITISHO NA MKUU WA MKOA

Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”

Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

MAGAZETI YA LEO APRIL 26 2013.

.
.
.
.
.
.

Madawa ya kulevya yakamatwa katika basi la ziara la mwanamuziki Justin bieber.


Polisi wa nchini Sweden wamedai kupata dawa za kulevya katika basi linalotumiwa na mwanamuziki Justin Bieber anapofanya ziara zake za kimuziki.
Msemaji wa polisi Lars Bystrom amesema kiwango kidogo cha dawa za kulevya na silaha moja vimekutwa katika basi hilo wakati polisi walipolivamia likiwa halina mtu na kuegeshwa katika ukumbi wa Globen mjini Stockholm ambapo mwanamuziki huyo alikuwa akifanya shoo.
Polisi huyo amekata kutaja aina ya dawa zilizokamatwa akisema zimepelekwa maabara kwa uchunguzi.
Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...