Friday, April 26, 2013

Madawa ya kulevya yakamatwa katika basi la ziara la mwanamuziki Justin bieber.


Polisi wa nchini Sweden wamedai kupata dawa za kulevya katika basi linalotumiwa na mwanamuziki Justin Bieber anapofanya ziara zake za kimuziki.
Msemaji wa polisi Lars Bystrom amesema kiwango kidogo cha dawa za kulevya na silaha moja vimekutwa katika basi hilo wakati polisi walipolivamia likiwa halina mtu na kuegeshwa katika ukumbi wa Globen mjini Stockholm ambapo mwanamuziki huyo alikuwa akifanya shoo.
Polisi huyo amekata kutaja aina ya dawa zilizokamatwa akisema zimepelekwa maabara kwa uchunguzi.
Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...