Friday, April 26, 2013

WASANII WALIPONDA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA

BUNGE la Jamhuri la Muungano wa Tanzania limeonekana kuwachosha baadhi ya wasanii kutokana na kukosa hoja za maana za kujadili ndani ya bunge hilo na matokeo yake kuwa kama kijiwe kwa kutumia lugha chafu zilizokosa tija kwa taifa

Kutokana na hali hiyo ya baadhi ya wabunge kukosa lugha na sera zenye tija wawapo bungeni baadhi ya wasanii wanaliona hilo ni moja ya changamoto inayosababisha watanzania kuzidi kuwa na hari ngumu ya kimaisha kwa kukosa watetezi wenye umakini

Mmoja wa wasanii hao akizungumza na jarida hili Ben Pol alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wabunge kutumia lugha ya matusi  kwenye kujadili hoja na matokeo yake wanashindwa kupata muafaka wa wanayo yajadili

Alisema kuwa bunge limekosa muelekeo na ameacha kulisikiliza bunge hilo kwa sababu ya kukosa mueleko na kujaa lugha chafu za matusi huku wakishindwa kuyajadili yale ya msingi kwa taifa lao

Kutokana na hali hiyo nchi ya Tanzania itaendelea kubaki maskini na vitu kuendelea kupanda bei kila siku huku kipato cha wananchi kuwa duni kwa kukosa watetezi

Alisema kuwa bunge halijafika sehemu nzuri na kuonekana halina tija kwa wananchi wake na hali hiyo linasababisha wananchi kushindwa kupata ukombozi kwa yale wanayoyakusudiwa

Kwa upande wake msanii wa filamu nchini Rose Ndauka alisema kuwa bunge limekuwa si la wastaarabu na matokeo yake wanajadili vitu ambavyo havina tija kwa jamii

Alisema kuwa Tanzania ni nchini ya wastaarabu na wajadili vitu vya ustaarabu kwa kufikia muafaka hali hiyo imekuwa tofauti sasa kwa baadhi ya wabunge kujadili vitu kwa lugha chafu hali inayoshangaza taifa

"Wananchi tumewachagua wabunge huku tukiamini kuwa watafanya hilo tulilowaagiza ila hali imekuwa tofauti na mika mingine baadhi ya wabunge kuanza kujadili vitu visivyo na tija kwa wananchi wao" alisema Ndauka

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...