Habari Habari za uhakika zilieleza kuwa Wema na timu ya wafanyakazi
katika kampuni yake ya Endless Fame Production, alikodisha ndege ya
kifahari kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya mapumziko tangu Aprili 18
hadi 20, mwaka huu.
Ilifahamika kuwa
ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na
kampani yake tu.
CHANZO
CHA YOTE NI DIAMOND
Ilibumburuka kuwa
timu yake hiyo ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda
kwenye mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.
Ilielezwa kuwa stresi alizokuwa nazo
zilitokana na ile ishu ya kudaiwa kurekodiwa akibembeleza penzi kwa
aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku mkali
huku jamaa akiwa amelala na mpenziwe wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya kutokea
kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza
mawazo.
“Unajua ile ishu ilimchanganya sana bidada maana
hakutegemea kama Diamond anaweza kufanya kitu kama kile so (kwa hiyo)
alikwenda kutuliza akili na kweli sasa hivi walau yupo fresh (vizuri),”
alisema sosi wa karibu wa Wema.
AINGIA ARUSHA KWA ULINZI MKALI
Walipoingia jijini Arusha, staa huyo wa Filamu ya The
Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika hoteli ya bei mbaya
aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege)
hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo
chetu,
APOKEA
MWALIKO
Habari zilieleza kuwa akiwa hotelini
hapo, habari zilienea kama moto wa kifuu kuwa yupo jijini Arusha hivyo
akapokea mwaliko kutoka kwa mashabiki wake waliotaka japo kumuona tu
kwenye Fashion Show iliyoandaliwa.
KASHESHE
‘Eventi’
ilifanyika kwenye Ukumbi wa Club D (World Garden) uliopo jijini humo na
ndipo kasheshe lilipoibuka kwa watu kukanyagana wakitaka kumuona na
kupiga naye picha.
“Aisee
Wema wee acha tu! Kusema kweli watu wanampenda sana. Kuna wakati niliona
kama ukumbi unakuwa mdogo na kwa taarifa yako ilikuwa haijatangazwa.
Sijui kama ingekuwa imetangazwa kuwa Wema yupo A-town, ingekuwaje maana
kila mtu alitaka japo amshike tu,” alisema sosi wetu huyo.
MENEJA
Kwa mujibu wa meneja wake, Martin
Kadinda, ilibidi kuomba ulinzi maalum wa mabaunsa ambao walihakikisha
hadhuriki.
“Tuliwaambia tupo
na mtu mkubwa sana hivyo tukapatiwa ulinzi maalum wa kuhakikisha Wema
hapati tatizo la mtu kumdhuru na ndicho tulichokifanya,” alisema
Kadinda.
Ilifahamika kuwa kwa harakaharaka ulinzi wa Wema
ulikuwa na takriban watu wasiopungua 10, yote ikiwa ni kuhakikisha
usalama wake.
AFANANISHWA
NA KIM KARDASHIAN
Kwa mujibu wa mashabiki wake ukumbini
hapo, ulinzi wa Wema ulifananishwa na ule wa staa wa Marekani, Kim
Kardashian ambaye hivi karibuni aliwekwa mtu kati na watu zaidi ya 32
wakiwemo askari na mabaunsa.
“Kweli
Wema sasa amefikia levo za akina Kim, yaani naye ana ulinzi mkubwa
hivi?” alihoji mmoja wa mashabiki wake.
TIMU NZIMA
Ukimwacha Wema na Kadinda, wengine
walioambatana nao ni Kajala Masanja, Petit Man ‘Wakuache’, Tinny Daddy
na Nurdin Bilal ‘Shetta’. Baada
ya mapumziko wote walirejea jijini Dar na kuendeleza libeneke wakiwa
‘wamerefreshi’ akili.
NI KUFURU
NYINGINE
Hii ni kufuru
nyingine ya Wema ambapo swali liliendelea kubaki palepale kuwa anapata
wapi fedha anazotumia katika matukio yake ya gharama kubwa huku nyuma
yake kukiwa na madai kuwa kuna ‘mkubwa’ mmoja anamuwezesha.
Na GPS
No comments:
Post a Comment