Taarifa
za sasa kutoka Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema
anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma
za uchochezi wa vurugu za Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa
Mkoa Arusha juzi.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mke wa Mh.
Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake na kusema
mpaka jumatatu ndio itajulikana.
Namkariri
Mke wa Lema akiongea na TheTZA millardayo.com akisema “jana usiku saa
sita kasoro watu walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende
kutazama ni kina nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na
tulikataa kwa sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka
kuitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa
nikifatilia gari mbona chochote hakikutokea?”
“Baada
ya muda kusogea ikabidi Lema aanze kuwapigia marafiki, jamaa na baadhi
ya viongozi wa Chadema, kabla ya hapo pia tuliamua kupiga kengele ya
kampuni ya security ambao muda mfupi baadae walikuja na gari yao huku
Polisi wakiendelea na vitisho kwamba watapiga mabomu na kuvunja ukuta la
sivyo Lema ajisalimishe, Viongozi wa Chadema na marafiki walipowasili
wakamshauri Lema ndio akajitokeza wakati huo ni saa tisa usiku” – Mama
Lema
“Alipojitokeza Polisi walimchukua na mimi nikaondoka nao,
tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa maelezo lakini alikataa na
kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa rumande, asubuhi
tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye kikao na
haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa
nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi
ikamalizika jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka
Jumatatu” – Mama Lema
“shitaka kubwa lililo mbele yake ni
uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo cha
Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye
maelezo Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi
kubwa kuliko zote ni uoga” – Mama Lema
Kwa
kumalizia, Mke wa Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa
na Polisi tumerudishiwa baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale
waliolivuta, gari liko zima kabisa………… toka nimeolewa na Lema
nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake ya kwanza
kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za Ubunge”Kwaisani ya
Millard Ayo
No comments:
Post a Comment