Baada ya msiba wa
Bi Kidude kumalizika, hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond’ alibaki peke yake na mwili wa marehemu chumbani
kwa ajili ya kuchota nyota ya Bi. Kidude.
Leo tunaye Dr
Salum Mkumba ambaye ataeleza kwa kirefu tafsiri ya kitendo alichokifanya
Diamond.
Funguka: Dr Mkumba asalam aleikum, karibu ndani ya nyumba
kubwa ya magazeti Pendwa Tanzania, Global Publishers Ltd.
Dr Mkumba:
Waaleikum salaam, ahsanteni nashukuru. Mimi leo nina jambo ninataka
niliweke sawa.
Funguka: Liweke sawa, sisi pamoja na wasomaji wetu wa
Risasi Jumamosi tunakusikiliza.
Dr Mkumba: Nataka kuweka sawa juu
ya suala la nyota, mtu akifariki huwa anakwenda na nyota yake sasa
nimeshangaa kusikia Diamond alikwenda kuchukua nyota ya marehemu.
Funguka: Sasa Diamond alipobaki peke yake chumbani na mwili wa marehemu
ilikuwa ina maana gani?
Dr Mkumba: Pale alikuwa anajaribu
kujisafisha tu katika jamii, hakuna cha ziada.
Funguka: Unaposema
anajisafisha, kwani amechafuka?
Dr Mkumba: Eee! Kwani hujui?
Amenaswa na mke wa mtu hotelini, skendo za wanawake tofauti zimekuwa
zikimtafuna kila kukicha.
Funguka: Unaposema alikuwa anajisafisha
una kitu gani cha kushika mkononi?
Dr Mkumba: Surat Nnajimi Sura ya
39 imezungumza kwa kirefu ila tafsiri yake ipo hivi; hakuna
anachokichuma mwanadamu kwa marehemu ila marehemu anategemea kuombewa
dua na mtu mzima.
Funguka: Kwa hiyo ina maana vile alivyofanya
Diamond ni kazi bure?
Dr Mkumba: Nakwambia hakuna cha maana zaidi ya
kujisafisha.
Funguka: Sasa una mshauri nini Diamond?
Dr
Mkumba: Amrudie mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada ya kweli.
Funguka:
Vipi kuhusu suala la kujenga msikiti ambalo Diamond alitangaza kuwa ana
mpango huo?
Dr Mkumba: Hapo ndiyo kabisa, ajenge tu lakini haisaidii
kitu sababu ukijenga nyumba ya ibada inatakiwa utumie fedha ambazo
umezipata kihalali katika njia safi.
Funguka: Kwani fedha zake
hajazichuma kwa njia safi?
Dr Mkumba: Kiimani yetu ya Kiislam muziki
siyo halali hivyo fedha anayoipata kwenye muziki haiwezi kuwa halali.
Funguka: Tunashukuru, karibu tena siku nyingine.
Dr Mkumba: Haya
Ishallah!
No comments:
Post a Comment