Tukio hilo la
kusikitisha lilitokea Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu katika chumba
namba 107 kwenye gesti iitwayo Jamboz iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Habari za uhakika zilieleza kuwa tukio hilo
lilikuwa ni mtego baada ya walezi wa denti huyo kunasa mawasiliano ya
mfanyabiashara huyo akimrubuni binti yao.
Katika mawasiliano
hayo, Tajiri alimtaka denti huyo wa sekondari moja iliyopo Kibamba, Dar
(jina linahifadhiwa kwa sababu maalum za weledi wa uandishi wa
habari), wakutane kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kuimomonyoa amri ya
sita.
Baada ya walezi hao kuufuma ujumbe kwenye
simu ya binti yao, walimuwekea doria bila mwenyewe kujijua na
ulipokaribia muda waliokubaliana kukutana gesti, denti huyo aliaga
anakwenda ‘tuisheni’.
Huku mwandishi
wetu wakiwa ‘stendibai’, kitendo cha binti huyo kuaga muda huo kilianza
kuonesha dalili za mtego wa walezi kukaribia kukamilika.
Waandishi wetu ndiyo waliokuwa wa kwanza kufika eneo la tukio
na kujibanza wakiwa na picha za wawili hao ambapo walimshuhudia
mfanyabiashara huyo akifika kaunta na kuagiza maji makubwa na kuyanywa
hadi yakaisha kisha kuelekea kwenye dirisha la mapokezi ya gesti hiyo.
Ilidaiwa kuwa yale maji aliyokunywa chupa
nzima alilenga kuwa fiti kwa ajili ya ‘gemu’ na ‘kadenti hako’.
Mmoja wa waandishi wetu naye alijisogeza kwenye dirisha hilo akijifanya kutaka chumba na kumsikia mhudumu akimpa Tajiri chumba namba 107 na kumuonesha kilipo.
Ghafla binti
huyo naye alifika mapokezi akiwa na sare za shule ambapo alimkuta
paparazi wetu akiendelea kuzuga kwa kutaka kukagua chumba kizuri kabla
ya kulipia.
Dakika chache baada ya Tajiri na denti huyo kuingia chumbani,
mwanausalama mmoja alitangulia akifuatwa na mwandishi wetu na ndugu wa
denti huyo ambapo waliomba kukagua chumba hicho kwa kuwa kulikuwa na
binti yao.
Waliporuhusiwa waliingia na kugonga chumba
ambapo jamaa huyo alifungua, wote wakakutwa wakiwa watupu huku
mfanyabiashara huyo akiwa kwenye harakati za kuvaa ‘kinga’ au ‘dawa ya
penzi’ baada ya kumchezea mtoto wa watu.
Tukio hilo
lilivuta hisia za jazba kwa umati uliofurika ghafla kwenye eneo hilo
huku kila mtu akilaani kitendo cha jamaa huyo kumkatishia denti huyo
masomo na kumpeleka gesti kwa ajili ya ngono.
“Fikiria wewe kama mzazi unalipa ada mtoto wako asome halafu
mtu mwingine kwa makusudi anamwachisha masomo na kumpeleka gesti
wakafanye ngono! Kweli inauma sana, kila mzazi anatokwa na machozi,”
alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuibuka kwa varangati
gesti hapo.
Kwa upande wake, dada mlezi wa anayemsomesha denti huyo (jina tunalo) alijikuta akimnasa makofi mfanyabishara huyo na kuzua timbwili zito kutokana na kupandwa na hasira ya ajabu.
Katika vuta nikuvute, ghafla jamaa huyo alifanikiwa
kuwachoropoka na kuingia mitaani akitimua mbio hivyo kutoa kazi
nyingine ya kuanza kumsaka upya ili afikishwe kwenye mkono wa sheria.
No comments:
Post a Comment