Tuesday, April 02, 2013

MAGAZETI YA LEO APRIL 2, 2013

..
..
..

KIJIJI CHA MISUKULE CHAGUNDULIWA NCHINI

Msukule.


Msukule.
Msukule.



Na Makongoro Oging', Bagamoyo


INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo  mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi  wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.

Uchunguzi umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa kimazingara.
Imebainika kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.

AGNES MASOGANGE AWEKA PICHA INSTRAGRAM AKIWA KATIKA POZI ZA KIMAHABA

Ni miezi michache imepita tangu video queen wa bongo Agnes Masogange aadhirike baada ya video yake chafu kusambaa ikionesha waki**** na jamaa yake.
 
Lakini sasa inaanza kuonekana kuwa dada huyu hii ni michezo yake baada leo kupost picha zinazomuonesha wakiwa kimahaba na mpenzi wake katika mtandao wa instragram.JE HIVI TUKIONA VIDEO NYINGINE AKIWA NA HUYU MCHIZI TUTASHANGAA AU TUTASEMA NDIO KAZI YAKE?

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR ALIGOMBEA UBUNGE TIKETI YA CUF 2010

IMEELEZWA kuwa, mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35) anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumuua Padri Evaristus Mushi ni mwanachama wa CUF ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika Jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud alithibitisha jana kuwa, mtuhumiwa huyo ni mwanachama wao na alishiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu na kusimamishwa na chama katika kampeni za Uwakilishi Jimbo la Rahaleo.
“Ni kweli mtuhumiwa anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padri Mushi ni mwanachama wetu na alishiriki katika mchakato wa kuwania Uwakilishi Jimbo la Rahaleo mwaka 2010.
Hata hivyo, Hamad alisisitiza na kusema suala la Omar kamwe lisihusishwe na CUF na kusema suala hilo watalitolea tamko baadaye.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ripoti ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Jimbo la Rahaleo, mgombea wa CCM, Nassor Salim Ali maarufu kama Jazirra aliibuka na ushindi kwa kupata kura 3,952 sawa na asilimia 63.10, wakati mgombea wa CUF, Omar Mussa Makame alipata kura 2,310 sawa na asilimia 39.9 na kushika nafasi ya pili.

RUNGWE MBEYA IMEENDELEA KUKUMBWA NA MATUKIO YA MAUAJI YA KUTISHA, TAHADHARI PICHA HIZI ZINATISHA.....!!



TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZINAZOONEKANA ZA MTOTO AYUBU HAPA NICHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU




KUSHOTO NI BABA MZAZI WA AYUBU AGEN MWAKALEGELA AKIWA NA NDUGU ZAKE WAKISUBIRI KUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU AYUBU

Rais Jakaya Kikwete Akutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Monday, April 01, 2013

Mgodi wafukia wachimbaji Arusha; zaidi ya watu 18 wanahofiwa kufariki.. Wanajeshi wafanaya uokozi sasa na tayari mtu mmoja ameokolewa hai na wengine watatu wakiwa wameshakufa

ajali (55)
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema 
ajali (66)



Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo

KAMANDA MPINGA MATATANI

ADAIWA KUAMURU GARI LILILOBEBA MAZAO YA MISITU LIACHIWE.

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga ameingia kwenye kashfa akidaiwa kuamrisha askari wa kikosi hicho mkoani Singida kuliachia gari lililokamatwa usiku likiwa na shehena ya mazao ya misitu juzi.

Kutokana na tukio hilo, askari mwenye namba D.9523 Koplo Azizi wa kituo kidogo cha polisi Ikungi mkoani Singida ameingia matatani baada ya kulikamata gari hilo lenye namba za usajili T 271 BTR na trela namba T 686 BTX lenye urefu wa futi 40.

SIMULIZI YA ALIYENUSURIKA KIFO KUTOKA GHOROFA YA 15.


Fundi ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
 

Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16. Picha na Muhidin Michuzi. 


FUNDI ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.


Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini kwamba kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi akiendelea na ujenzi.

Alieleza kuwa hakuwa anafahamu kinachoendelea, bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko hospitalini.

OBAMA AENDA KANISANI KWA MIGUU NA FAMILIA YAKE SIKU YA PASAKA, TAZAMA PICHA HAPA

Rais Barack Obama akitembea kwa miguu na Familia yake kutoka White House across Pennsylvania Ave.  hadi Lafayette Park. huku akiwa amemshikili mtoto wake wa pili Sasha mkono pamoja, Mkewe Michelle Obama  na binti yao mkubwa Malia kuelekea katika Kanisa la St. John’s Episcopal liliopo Washington, DC ambapo walihudhuria  katika Pasaka  Siku ya Jumapili Machi 31, 2013. ( Official White House Picha na Pete Souza)

Pastor at Obamas Easter Church Service: Captains of the Religious Right Want Blacks in the Back of the Bus, Women Back in the Kitchen
Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama walipotembea kutoka White House na binti zao Sasha Obama, wa pili kutoka kushoto, na Malia Obama, kulia, wakitembea kwa miguu kupitia Lafayette Park kwenda  katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington. (AP)

Obama alipokua akitembea Mitaa ya Lafayette Park  hadi  St. John's Episcopal Church Siku ya Jumapili  , March 31, 2013, ndani ya Jiji la Washington. (Picha na Carolyn Kaster)
OBAMAEASTER1N_2_WEB
Obamas akitembea kupitia Lafayette Park kwenda Kanisasani  kwajili ya Pasaka.
OBAMAEASTER1N_4_WEB
Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake walipo maliza ibada katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington.

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013


Ndugu Wananchi;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi.  Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania
Ndugu wananchi; 
Jambo la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013.  Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania.  Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake.  Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.

MKAPA ASEMA:TUSITANGULIZE UDINI KWENYE KATIBA


Ujumbe wa amani na tahadhari ya umakini kwenye utoaji maoni kwenye Katiba ndiyo vilitawala wakati wa misa za Sikukuu ya Pasaka zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini jana na juzi. 
Miongoni mwa waliotoa hotuba wakati wa sikukuu hiyo ni 
pamoja na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alikuwa mkoani Mtwara; na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyekuwa jijini Dar es Salaam. 
Mkapa akataa udini 
Rais mstaafu Mkapa alitumia fursa ya kutoa salamu katika Kanisa Katoliki mjini Masasi kuliasa taifa kujiepusha na utoaji wa maoni ya Katiba kwa misingi ya dini. 
Mkapa alisema katiba ijayo haipaswi kuwa na itikadi za kidini kwa kuwa zinaweza kuliangamiza taifa.

WANAUME BONGO MOVIE HAWANA MAPENZI YA KWELI: SNURA

MKALI wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi amesema anaogopa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu kwani wengi wao hawana mapenzi ya kweli.
 
Akipiga domo na paparazi wetu, Snura alisema tangu aanze kucheza filamu alijiapiza kuwa kamwe hatajiingiza kwenye mapenzi na waigizaji zaidi ya kushirikiana nao katika kazi ya kuzalisha filamu.
“Mimi siwapendi wanaume wasanii wa filamu, sijawahi kuwa nao labda awe msanii wa Bongo Fleva,” alisema Snura.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 01.04.2013

.
.
.
.
.
.

MAKAHABA RAIA WA RWANDA MATATANI DODOMA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi1tiX0ExlorOYy5PlS5BybXxR-RE62-JNK58tvu27-tZ3kOtyvmVN2ONaQvBZkjXobq3njO7egLEHYvTvkYpM6sK3IVK9LvhxlzFp9Msw1t8IgR6jC29Sw0C4juffM53C24B3FetSfhoQ/s1600/changudoa+%281%29.jpg
WANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...