Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.Picha na
IKULU
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Akiongea
na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama
ya Serengeti mkoani Mara, Rais Kikwete amempongeza Mhe Ruto na Rais
mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi
mkuu nchini Kenya.
Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.
Alielelezea
matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya
utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Mhe
Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na
watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na
mwenyeji wake.
Mwisho
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Aprili, 2013
No comments:
Post a Comment