MWILI
WA ALIYETUHUMIWA KWA MAUAJI YA MTOTO AYUBU AGEN UKIWA UMECHOMWA MOTO
NAWANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMKUTA MITA CHACHE KUTOKA KWENYE
MWILI WA MAREHEMU AKIWA NA KISU KINACHODHANIWA KUTUMIKA KATIKA MAUAJI
|
MWILI WA MTOTO AYUBU UKITOLEWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANAWILAYA YA RUNGWE |
SAFARI YA KUELEKEA KIJIJI CHA IJOKA KWA MAZISHI
-wananchi wapanda hasira wamteketeza kwa moto mtuhumiwa.
MATUKIO
ya kutisha na ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa
Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa
kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata
hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa
wa tukio hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo
baada ya kummbana ili aeleze sehemu walikokificha kichwa cha marehemu
aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.
Habari
za uhakika kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa
kijiji cha Ijoka katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael
Mwaikenda, zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa
11:00 jioni.
Akifafanua
zaidi Mwenyekiti huyo alisema, marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi
wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba
alikutwa na mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika
kufanikiwa kumuiba nyumbani kwao.
Mwaikenda
alisema mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na
kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi
tu baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa
marehemu .
“Marehemu
alichukuliwa na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na
wenzake baada ya kuona hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi
walianza kumtafuta bila mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea
na harakati hizo waliukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa kichakana na
wauaji hao kuondoka na kichwa” alifafanua Mwaikenda.
Mkazi
mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo,
alisema baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea
kuwasaka wahusika na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na
mtu mmoja ambaye walimtilia mashaka.
Alisema
baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na
mgeni kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira
wananchi jambo lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua
papo hapo.
Hata
hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo
licha ya kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa
kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa
wameondoka.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani
Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa
kichwa cha marehemu huyo hakijaonekana na jeshi hilo linaendelea
kufanya uchunguzi.
“Ni
kweli tukio hilo limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki
mauaji hayo naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira ambao
licha ya kumuua waliuteketeza mwili wake kwa moto”.
Aliongeza
kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka
kati ya 30 hadi 35 na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha
mauaji hayo kinahusishwa na imani za kishirikina.
Wakati
huo huo watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa
vibaya, katika matukio mawili tofauti ya ajili za barabarani mkoani
hapa.
Katika
tukio la kwanza lililotokea eneo la Mbalizi wilayani hapa, majira ya
saa nne usiku katika barabara ya Mbeya- Tunduma, watu wawili, Meshaki
Inkuru (24) na Said Ndasi (19) baada ya gari aina ya Toyota Chesser
yenye nambari za usajili T 516 AAA lililokuwa likiendeshwa na mtu
asiyefahamika kuwavamia wakiwa nje ya Hoteli ya Royal Tughimbe
walikokuwa wakiendelea na sherehe za Pasaka.
Kamanda
wa polisi aliwataja majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa katika
Hospitali teuli ya wilaya ya Mbeya ya Ifisi ni Shar Mkumbwa (20),
Juliet Katemi (18) wote wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi.
Tukio
lingine ni lile lililotokea eneo la Soweto ambapo mtu mmoja mtembea
kwa miguu, aliyetambuliwa kwa jina moja la Paul (60) kufa papo hapo
baada ya kugongwa na gari ambayo hata hivyo haikuweza kufahamika mara
moja .
SOURCE MBEYA YETU
|
No comments:
Post a Comment