Wagonjwa wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Nyakabale
mkoani Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza juzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua madaraka Mganga
Mkuu wa Zahanati ya Nyakabale, Josephat Msafiri kwa kukiuka miiko ya
kazi yake na kulewa wakati wa kazi.
Mkurugenzi huyo aliamua kuchukua uamuzi huo jana
kutokana na tukio lililotokea Juzi hii la daktari huyo kufunga kituo cha
afya na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa, kisha kwenda kunywa pombe
jambo lililowalazima kumchapa viboko akiwa baa.
“Tumeshamchukulia hatua za kinidhamu ikiwa ni
pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa
Serikali,” alisema Nakainga.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.