Tuesday, December 23, 2014

PHIRI AOMBA MIAKA MIWILI


Kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri amesema iwapo klabu yake itamvumilia kwa miaka miwili atatengeneza wachezaji bora kama ilivyo kwa nyota wa TP Mazembe ya DR Congo (DRC), Mbwana Samatta.

Phiri alisema: “Najivunia mafanikio ya Samatta (Mbwana). Kwanza yanatokana na uvumilivu wake na kujituma kwake pamoja na kupewa nafasi. Naamini makocha wanapopewa muda na timu wanaweza kutengeneza wachezaji wapya na hata kuinufaisha klabu kwa kuuza wachezaji hao kwa bei nzuri huku ikiendelea kutengeneza wengine.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

 

“Kama Simba itanipa muda wa hata miaka miwili nitafanya kazi kubwa, kwanza kuitafutia Simba ubingwa, pia kuifanya Simba kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa, lakini pia itapata fursa ya kuuza wachezaji na kupata faida kubwa.

“Unajua mchezaji kama Samatta alipitia kwenye mikono yangu na kwa uwezo alionao kwa wakati huo kuna wachezaji wengi wa sasa pia wanao, kinachoweza kuwasaidia mimi kukaa nao na muda wa kuwafundisha.

Kabla ya kusajiliwa TP Mazembe, Samatta alitokea Simba akiwa mmoja ya wachezaji waliotokea kwenye mikono ya Phiri wakati huo akiwa kocha.

Samatta aliichezea Simba kati ya 2010 na 2011 wakati Phiri mara ya kwanza aliifundisha Simba kati ya 2003 na 2005, kisha 2008 hadi 2011 na kurejea mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Phiri amekoshwa na uwezo wa beki Hassani Kessy aliyesajiliwa na timu hiyo mwishoni mwa dirisha dogo la usajili na kudai kuwa atakuwa hazina kubwa kwa timu hiyo na taifa kwa siku za usoni.

Alisema Kessy ana kasi na akili ya kufanya uamuzi wa haraka, kitu ambacho wachezaji wengi wa Kitanzania hawana.

“Kessy bado ni kijana mdogo lakini anaonyesha kuwa ameimarika upesi kisoka. Nimemtazama kwa muda mfupi nimegundua kuwa tumepata chaguo sahihi kwenye nafasi yake.”

Beki huyo aliyesajiliwa kwa Sh35 milioni kutoka Mtibwa Sugar, alionyesha kiwango kikubwa katika  dhidi ya Mwadui FC, wakati Simba ikiiibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Mwananchi 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...