Tuesday, December 23, 2014

YANGA KWA WANAJESHI, AZAM SUDAN

Mabingwa wa Tanzania, Azam wataanza harakati zake za Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa kuivaa El Merreikh ya Sudan, wakati Yanga wenyewe watakuwa na kibarua kwa BDF ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) inaonyesha wawakilishi wa Tanzania wataanzia nyumbani katika michezo yao itakayopigwa Februari 13, 14, 15 na mechi za marudiano zitakuwa kati ya Februari 27, 28 na Machi Mosi 2015.

Azam itawakaribisha El Merreikh na kurudiana wiki mbili baadayezijazo nchini Sudan na endapo itafanikiwa kushinda mechi hiyo katika hatua ya 16 bora itacheza na mshindi kati ya Lydia Ludic B.A (Burundi) au Kabuscord do Palanca (Angola).
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Wakati wawakilishi wa Zanzibar, mabingwa KMKM wenyewe wataanzia ugenini kwa kuvana naifuta El Hilal ya Sudan na endapo itasonga mbele fanikiwa kushinda katika 16 bora itacheza na mshindi kati ya Fomboni Club (Comoro) au Big Bullets (Mali)

Katika Kombe la Shirikisho CAF, vigogo wa soka nchini, mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga watakuwa nyumbani kuwakaribisha BDF ya Botswana kabla ya kurudiani jijini Gaborone wiki mbili baadaye.

Endapo Yanga itafanikiwa kushinda michezo hiyo miwili, itakutana na uo katika raundi ya 16 bora itacheza na mshindi kati ya Sofapaka (kenya) na Platinum (Zimbabwe) katika hatua ya 16 bora.

Wawakilishi wa Zanzibar, Polisi watacheza na CF Mounana (Gabon) na endapo watasonga mbele kifanikiwa kusonga mbele watacheza na mshindi wa mchezo kati ya Khartoum ya Sudan na Power Dynamos ya Zambia.

Mechi za raundi ya 16 bora zitachezwa kati ya Machi 13, 14, 15 na marudiano itakuwa Aprili 03, 04, 05, wakati mechi za hatua ya robo fainali 8 bora hatua ambayo itatoa timu zinazofuzu kwa hatua ya makundi zitafanyika Aprili 17, 18, 19 na mchezo wa marudiano utakuwa Mei 01, 02, 03 mwakani.

Katika Kombe la Shirikisho CAF raundi nane8 bora, mechi za kwanza zitafanyika Mei 15, 16, 17 na marudiano itakuwa Juni 05, 06, 07.

Wafalme wa soka barani AfrikaMabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa CAF, ES Setif hawataanzia raundi ya awali pamoja na Coton Sport, AC Leopards, Al Ahly, TP Mazembe na miamba ya Tunisia, CSS na EST.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...