Monday, December 22, 2014

"WATANZANIA KUNUFAIKA NA AJIRA QATAR" PINDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Watanzania watanufaika na kipato na maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira, ambazo watapata katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla, Pinda alisema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi hii inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni wachache.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
 

“Hivi sasa wapo Watanzania wanaofanya kazi hapa, lakini ni wachache mno. Mazungumzo yalishaanza siku za nyuma. Tukisaini mkataba katika muda mfupi ujao, tutajua ni idadi gani wanahitajika na wanaweza kuja kila baada ya muda gani,” alifafanua Waziri Mkuu.
“Hapa Qatar kuna uwekezaji mkubwa umefanyika, kwa hiyo wanahitaji watu wa kufanya kazi kwenye mahoteli, viwandani, na kikubwa hapa ninachokiona watu wetu watapata kipato, lakini pia watapata ujuzi kwa maana ya maarifa yanayoendana na teknolojia ya kisasa,” aliongeza.
Akieleza mambo mengine ambayo wamekubaliana kushirikiana kama nchi rafiki, Waziri Mkuu alisema kuna mambo makuu manne likiwemo hilo la ajira.
“La kwanza ni kilimo. Hapa Qatar ni jangwa kila mahali. Wamekubali kuja kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwa sababu sisi tuko karibu nao zaidi kuliko Marekani au Brazil,” alisema.
“Wanaweza kupata mchele, matunda, nyama kwa maana ya machinjio na viwanda vya kusindika nyama, lakini pia katika uvuvi wa samaki. Tunayo bahari ila mitaji yetu ni midogo. Kwa hiyo wamekubali kuangalia eneo hilo pia,” alisema.
Alisema eneo la pili ni la gesi na mafuta. “Wamekubali kutusaidia utaalamu ili tushirikiane nao katika namna ya kutumia gesi kwenye ngazi ya chini hasa viwanda kwa sababu wenzetu wana uzoefu wa muda mrefu. Hata kwenye mafuta wameonesha kuwa wako tayari,” alisema.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Habari Leo 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...