Monday, December 22, 2014

KIKWETE "HATUWEZI KUENDELEA KWA KUTEGEMEA RAMLI"

Sehemu ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru, Arusha

Sehemu ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru Arusha.

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa kamwe Tanzania, kama ilivyo nchi nyingine yoyote duniani, haiwezi kuendelea kwa kutegemea mazingaombwe ama ramli bila kuwekeza kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, ametaka Watanzania kuacha mwenendo wa kutumia ubishi wa kisiasa kutafuta majawabu ya changamoto za maendeleo akisisitiza kuwa majawabu ya maendeleo yatapatikana katika maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Amewataka Watanzania kuongeza kasi yao ya matumizi ya intaneti akisema kuwa mfumo huo wa habari na mawasiliano ni chimbuko kubwa la elimu ikiwemo elimu ya sayansi kuliko kutegemea kupata elimu hiyo katika magazeti.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru, Arusha, taasisi ambayo hutoa shahada za juu za uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi.
Akizungumza baada ya yeye mwenyewe kuwa ametunukiwa Digrii ya Heshima ya Uzamivu (PhD Honoris Causa) katika mahafali hayo ya pili, Rais Kikwete alielekeza sehemu kubwa ya hotuba yake kuelezea umuhimu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia katika uhai na maendeleo ya Tanzania na taifa lolote duniani.
“Somo tunalolipata ni kwamba hakuna mazingaombwe wala njia ya mkato ya kujipatia maendeleo ya juu. “Hatuna budi kuwekeza katika kuendeleza sayansi na teknolojia nchini, kama kweli tunataka kutoka hapa tulipo. “Hakuna ramli wala pumba za uchawi zinazoweza kuendeleza nchi yetu hata ukiimwaga pumba hiyo katika kila njia panda ya barabara na sehemu zote za Tanzania. Bado Tanzania haitabadilika hata inchi moja,” alisema Rais Kikwete na kuongeza: “Hatuna budi kuwekeza zaidi katika kufundisha wanasayansi, na katika tafiti na ujenzi wa miundombinu ya kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti zao. Kwa muda mrefu sana hili ni eneo ambalo hatukulipa uzito unaostahili.”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...