Tuesday, December 23, 2014

RAIS KIKWETE: FEDHA ZA TEGETA ESCROW NI ZA EPTL

Rais Jakaya Kikwete akihutubira wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa.

Rais Jakaya Kikwete amesema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa zinafikia Sh306 bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.
Akijibu swali alilojiuliza mwenyewe katika hotuba yake ya zaidi ya saa mbili kuwa: “Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL?” Rais Kikwete alisema kumekuwapo na maneno mengi, kila mtu anasema yake na wenzangu Wakwere tunasema ‘tunazoza sana’ akimaanisha waongea sana.
Alisema, “Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipoulizwa na Kamati ya Bunge alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL.
“Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikuwa wanalipa moja kwa moja kwa Tanesco lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke Benki Kuu ya Tanzania (BoT).”
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Akielezea maana ya escrow, alisema, “Ni tofauti kidogo na akaunti zetu tatu tulizozizoea, ni akaunti maalumu ya kazi maalumu na kazi hiyo maalumu ikiisha inafungwa. Inasimamia na wakala na wakala pia ana jukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.”
Ukumbi uliojaa wazee na wasio wazee wakimsikiliza kwa umakini ulikuwa umetulia kimya alipoanza kuzungumzia sakata hilo, akisema akaunti hiyo ilifunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka fedha za tozo ya uwekezaji, ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao.
“Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya Tanesco yakakubaliwa na tozo kupunguzwa, katika kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za Tanesco ambazo lazima zirudi, bahati mbaya miaka saba baadaye hilo (la maelewano) halikuwa limefanyika.”
“Kama katika fedha hizo ipo kodi ya Serikali na kwa mujibu CAG kulikuwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikuwa zaidi ya Sh21.7 bilioni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepeleka madai yake kwa PAP,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza: “CAG aliwaelekeza Tanesco kuacha kuhesabu fedha walizolipa kwenye Akaunti ya Escrow kama yao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya Tanesco. Mahakama Kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na Mahakama ikakubali.”
Alisema Wizara ya Nishati na Madini ilimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (wakati huo), Jaji Frederick Werema kuomba ushauri na aliwashauri; “walipeni, uamuzi uko sawa na hauna matatizo na BoT waliuliza maswali hayohayo na majibu yakawa yaleyale.”
Alisema: “Kwa kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa PAP. Mjadala ukaendelea bungeni na kwenye mablogu. Hata Tanesco ilipewa ushauri huohuo, uamuzi ule umetiliwa shaka na kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu kunufaika binafsi. Mara kuna watu wamekwenda benki na kubeba pesa viroba, kwenye sandarusi, lumbesa na mengineyo.”
Alisema, “Nilipokutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala Mahakama haikufanya makosa na huo ndiyo ulikuwa msimamo wake na mpaka sasa bado anaamini hivyo kuwa fedha si mali ya umma.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.


“Kuhusu hasara iliyopatikana alisema hakuna hasara yoyote iliyopatikana kwa sababu fedha ililipwa kwa mtu halali. Kwa upande wa kodi ya Serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa. Yamesemwa mengi na bado hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa walizozipata wazipeleke Takukuru. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...