Tuesday, March 27, 2018
MABALOZI WA URUSI WAFUKUZWA KATIKA NCHI MBALIMBALI
Australia imekuwa nchi ya karibuni kufukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya.
Waziri mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara mwisho vita vya pili vya dunia.
Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi kubwa kuwahi kutokea katika historia. Zaidi ya nchi 20 zimeungana na umoja wa Ulaya kuwafukuza zaidi ya wanadiplomasia 100.
URENO YA CRISTIANO RONALDO WAPIGWA 3-0 NA UHOLANZI
Mabingwa wa Ulaya Ureno walipokezwa kichapo cha kushangaza na Uholanzi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezewa mjini Geneva, Uswizi.
Winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel waliwaweka Waholanzi 2-0 mbele.
Beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ambaye majuzi alitawazwa nahodha mpya wa timu hiyo, alifunga la tatu.
BRAZIL KULIPIZA KICHAPO CHA 7-1 AU KUAIBISHWA TENA?!
Mkufunzi wa Brazil Tite amesema timu yake bado inatatizwa na "mizimu" ya kipigo cha 7-1 ambacho walipokezwa na Ujerumani katika nusu fainali ya Kombe la Dunia miaka minne iliyopita.
Mataifa hayo mawili yatakutana tena mara ya kwanza Jumanne mjini Berlin tangu Brazil walipoaibishwa kwao nyumbani wakati wa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
"Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia hakuna anayehitaji kujidanganya kuhusu hilo," Titea aliambia jarida la Kicker.
Monday, March 26, 2018
SIMBA NA YANGA KUKUTANA TAREHE HII HAPA
Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura leo imetangaza rasmi
tarehe ambayo Watani wa Jadi (Simba SC na Yanga SC) watakutana kucheza mechi
yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wambura
amesema timu hizo sasa zitacheza tarehe 29 Aprili 2018 katika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam katika mechi ambayo Simba atakuwa mwenyeji wa pambano hilo. Awali
Bodi ya Ligi ilikuwa haijaweka tarehe hiyo wazi kutokana na mambo mbalimbali
kuingiliana na kufanya ratiba ya mchezo huo kutopangwa kwa wakati.
Timu
hizi zenye wafuasi wengi nchini, zilikutana Oktoba 28 2017 kwenye mzunguko wa
kwanza wa ligi na kwenda sare ya bao 1-1, huku wafungaji wa mabao hayo wakiwa
ni Shiza Kichuya upande wa Simba na Obrey Chirwa kwa Yanga.
Pamoja
na michezo mingine mbalimbali ambayo leo imetolewa ratiba yake rasmi, klabu ya
Simba imepangwa kucheza;
Njombe
Mji FC Vs Simba April 3
Mtibwa vs Simba Aprili 9
Lipuli FC vs Simba Aprili 20
Simba vs Yanga Aprili 29
NONDO AACHIWA HURU KWA DHAMANA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa leo Jumatatu, Machi 26, imemuachia Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania(TSNP), Abdul Nondo kwa dhamana ya Sh. 5 milioni na mali isiyohamishika.
Nondo amepewa dhamana hiyo mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia anayeendesha kesi hiyo baada ya mtuhumiwa kukamilisha taratibu zote za dhamana.
Wiki iliyopita, Nondo alinyimwa dhamana baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa ni kwa sababu za usalama wake.
Sunday, March 25, 2018
HUU HAPA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini huku akisikilizwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam Machi 27, 2016 (Picha na maktaba)
"Fumbua Kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao" (Mithali 31: 8-9)
Tunapoadhimisha sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tunatambua kuwa utume wa Kanisa letu katika taifa letu, unafanyika katikati ya changamoto kadhaa. Kwa kuwa Kanisa ni sehemu ya jamii, linaguswa na changamoto hizo.
Katika kukaa pamoja na kuliombea taifa letu, sisi maaskofu wa KKKT, tumetafakari na kubaini changamoto hizo. Kwa njia ya salaam za Pasaka, tunaleta kwenu changamoto tatu ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.
1. Jamii na Uchumi:
Kiini cha Utume wetu katika jamii kinatuingiza kwa nia njema katika maisha ya uchumi na mshikamano wa kijamii. Neno la Mungu linatufundisha kuwa "Mwanadamu hawezi kuishi kwa mkate peke yake" (Luka 4:4).
Saturday, March 24, 2018
VYUO 163 VYAFUNGIWA UDAHILI, VILIVYORUHUSIWA HIVI HAPA
BARAZA la Taifa la Elimu na Ufundi (Nacte) limezuia vyuo 163 kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada, baada ya kukutwa na upungufu ikiwako kutokuwa na walimu wenye sifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Machi 23 Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte, Dkt. Annastella Sigwejo amesema walifanya uhakiki kwa vyuo 459, kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa.
“Kutokana na hali hiyo hivyo ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu.”
Amesema licha ya kwamba vyuo vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa kuhakiki vyuo 459.
TGNP YAWAPA WAANDISHI WA HABARI MBINU YA KUEPUKA KUANDIKA HABARI ZA KICHOCHEZI
Bi. Mary Nsemwa mwezeshaji TGNP mtandao
Waandishi wa habari wamehimizwa kuandika habari za kijamii zinazowahusu wananchi moja kwa moja ili kuwasaidia wananchi kupaza sauti na kuepuka habari za kichochezi.
Mwezeshaji wa warsha ya mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Bi. Mary Nsemwa ameyasema hayo katika warsha iliyofanyika jana katika ukumbi wa Coffee Garden jijini Mbeya.
"Ukiandika habari zinazolenga maisha ya watu wa hali ya chini na kuibua kero zao huko vijijini hautaitwa mchochezi na ukizingatia Mh. amejipambanua kuwa yeye ni mtu wa watu maskini na ana nia ya kuwainua anaweza kufanya lolote katika kuwasaidia" alisema Bi. Nsemwa.
Wednesday, March 21, 2018
MAMBO 18 YA KUFANYA WAKATI WA MVUA ILI KUHAKIKISHA USALAMA WAKO
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha maeneo mengi Afrika Mashariki na kusababisha uharibifu wa mali na vifo. Huko nchini Kenya, watu zaidi ya 10 wamefariki baada ya kusombwa na maji ya mafuriko. Wakati hapa nchini Tanzania mvua hizo zimeleta maafa mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kukosa makazi n.k.
Wataalam wa masuala ya uoakoaji wametoa ushauri ambao unaweza kukufaa sana wakati huu wa mvua.
- Fahamu kwamba wakati wa kiangazi, vumbi, mchanga na taka za aina mbalimbali hurundikana barabarani. Mvua inaponyesha, husababisha barabara kuwa telezi na kwa hivyo ukiwa na gari ni muhimu kutoendesha gari lako kwa mwendo wa kasi kupindukia kwani gari likiteleza utashindwa kulidhibiti gari lako kwa urahisi. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KIGOGO WA SHIRIKA LEO MARCH 21
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Bi. Blandina Nyoni.
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu asubuhi ya leo March 21, 2018 inaeleza kuwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation – NHC) Bi. Blandina Nyoni kuanzia leo.
Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa Rais Magufuli ameivunja Bodi ya shirika hilo la NHC. Uteuzi wa Mwenyekiti mpya na bodi nyingine utafanyika hapo baadaye. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
HII NDIO TUZO NYINGINE ALIYOSHINDA CRISTIANO RONALDO
Mshambuliaji Real Madrid Cristiano Ronaldo
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora ya mwaka 2017 nchini Ureno.
Ronaldo
alitangazwa kupitia hafla iliyofanyika mjini Lisbon, baada ya
kuwashinda wachezaji Bernardo Silva wa Manchester City na kipa wa
klabu ya Sporting Lisbon Rui Patricio.
Ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real kushinda mataji yote ya
La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu
2017.
Naye Kocha wa klabu ya Monaco Leonardo Jardim ameshinda
tuzo ya kocha bora, baada ya kuiongoza timu hiyo ya Ufaransa kushinda
taji la Ligue 1 na kufika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa
Ulaya, wakati kocha wa Manchester United, Jose Mourinho akishinda tuzo
ya Vasco da Gama kwa kuitangaza vyema soka ya Ureno kimataifa.
Subscribe to:
Posts (Atom)