Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amesikitishwa
na matamshi ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakati
akihojiwa na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy, kwa hatua ambazo Wizara
inachukua kulinda maadili ya Kitanzania katika tasnia ya sanaa.
Maamuzi
ya kuzifungia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili,
yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza anayemlaumu. Diamond
atambue kuwa Serikali ina taratibu zake.
Maamuzi ya Naibu Waziri ni maamuzi ya Wizara.
Kama
ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao
hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular
he is. Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake,
nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa
Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea
wenzake.
Si
busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu
utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi
alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo.
No comments:
Post a Comment