Wednesday, March 21, 2018

HII NDIO TUZO NYINGINE ALIYOSHINDA CRISTIANO RONALDO


Mshambuliaji Real Madrid Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora ya mwaka 2017 nchini Ureno.

Ronaldo alitangazwa kupitia hafla iliyofanyika mjini Lisbon, baada ya kuwashinda wachezaji Bernardo Silva wa Manchester City na kipa wa klabu ya Sporting Lisbon Rui Patricio.

Ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real kushinda mataji yote ya La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu 2017. 

Naye Kocha wa klabu ya Monaco Leonardo Jardim ameshinda tuzo ya kocha bora, baada ya kuiongoza timu hiyo ya Ufaransa kushinda taji la Ligue 1 na kufika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, wakati kocha wa Manchester United, Jose Mourinho akishinda tuzo ya Vasco da Gama kwa kuitangaza vyema soka ya Ureno kimataifa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...