Thursday, May 05, 2016

MAN CITY WACHAPWA 1-0 NA REAL MADRID

 
Manchester City wameshindwa kufika katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.

Baada ya kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.
Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo. 

Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao 4,500.

Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. Real sasa watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...