Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akitoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya January Mosi hadi Aprili 12 mwaka huu, sawa na siku 102 vifo 969.
WAKATI ajali za barabarani zikiendelea kumaliza nguvu kazi ya Taifa
na kuumiza vichwa vya Watanzania kuhusu suluhisho la ajali hizo,
imefahamika moja ya tatizo sugu ni kukosekana kwa madereva wenye taaluma
stahiki, ingawa wana leseni.
Wiki hii peke yake, ajali tatu za mabasi zilizotokea Mbeya, Morogoro
na maeneo ya Mwanza, zimesababisha vifo vya watu 40 ndani ya siku sita.
Tayari Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga,
ametoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya
Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili 12, sawa na siku 102 vifo 969. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.