Wanawake wa UWT wakishangilia.
JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha,
imetangaza wazi kuwakataa walimu kusimamia uchaguzi wa madiwani, wabunge
na rais, kutokana na tabia ya kufanya hujuma kwa chama hicho wakati
wanasaidiwa mambo mengi ya msingi na serikali ya CCM.
Mbali ya walimu, pia UWT imewanyooshea kidole baadhi ya polisi mkoani
Arusha kwa kuwa na mapenzi yaliyopitiliza dhidi ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), hali inayowafanya kushindwa kutenda haki katika
maamuzi mbalimbali.
Msimamo huo umetangazwa kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa jumuiya
hiyo mkoa wa Arusha, Flora Zelote alipokuwa akizungumza katika kata
mbalimbali za wilaya ya Arusha katika ziara yake ya kikazi ya kukagua
uhai wa jumuiya hiyo na chama kwa ujumla. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Alisema kutokana na hali hiyo, jumuiya yake ina mpango wa kufikisha
mapendekezo yao kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na makao makuu ya
CCM ya namna ya kuwapata wasimamizi wengine wa uchaguzi mbadala wa
walimu hao.
Alisema CCM imeonekana kama mpangaji katika nyumba yake, kutokana na
mabaya yanayofanywa dhidi yake na watumishi wanaowalipa mishahara huku
chama hicho kikiendelea kukaa kimya.
“Polisi na walimu wanaolipwa mishahara na serikali ya CCM
wanakihujumu chama chetu, hii ni sawa na mwenye nyumba kugeuka kuwa
mpangaji au mke anayebaki kung’ang’ania cheti cha ndoa wakati nje
‘nyumba ndogo’ amemdhibiti mumewe.
Hii haiwezekani,” alisema Zelote. Alitumia nafasi hiyo
kuwatahadharisha viongozi wa Taifa wa CCM, kurejesha majina yale yale ya
wagombea watakayoyapendekeza mikoani, vinginevyo wakirejesha majina
mengine tofauti, watakuja kuwanadi wao katika kampeni.
Zelote alisema hali ilivyo sasa, chama kinapaswa kuheshimu matakwa ya
wananchi ya nani wanamtaka, badala ya kuendelea na tabia ya
kuwapendekeza watu kwa utashi wa kikundi cha watu, jambo ambalo
linasababisha ugumu katika kuwanadi wagombea hao.
“Mimi naomba nitoe msimamo wa jumuiya yangu mkoa wa Arusha, sisi
tutapendekeza wagombea kwa matakwa ya wananchi watakaowachagua na
tutawafikisha kwao ili wafanye maamuzi sahihi, wakifanya vinginevyo,
wakawaleta wa kwao, tutawapa taarifa waje kuwafanyia kampeni,” alisema
Zelote.
Alisema maamuzi hayo, pia yatafutwa katika ngazi ya wilaya, ambapo
vilevile kama wataacha mapendekezo ya kata zao na wakafanya vinginevyo,
nao watapewa taarifa kwenda kuwanadi wagombea waliowarejesha kwa utashi
wao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment