Mmoja wa manusura wa ajali iliyotokea eneo la Mto Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Mariam Manfredy akiwa amelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Mmoja wa majeruhi wa ajali iliyoua watu 19, Mariam Manfredy (28) aliyevunjika mguu wa kushoto, anasimulia ajali hiyo na kusema chanzo ni mwendo kasi na kuungua kwa breki.
Gari hilo lilikuwa ‘limeshona’ abiria, lilikuwa
likitoka jijini Mbeya kwenda Kiwira wilayani Rungwe kabla ya kuanguka
eneo la Mto Kiwira na kuua watu 18 palepale na mmoja alifia Hospitali ya
Igogwe huku wengine watatu wakijeruhiwa.
Mariam aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
(MRH), alisema alipanda basi hilo katika Kijiji cha Simambwe akienda
Kiwira kununua bidhaa za biashara. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Tulipofika Kijiji cha Ndaga, magurudumu yalianza kutoa cheche na moshi jambo lililomfanya kondakta kuteremka na kuzima kwa maji na kwamba wengi walisema breki zimeungua kwa kuwa kulikuwa na harufu kali ya kitu kinachoungua.
“Baada ya kuzima moto kwenye matairi hayo, dereva
aliendelea na safari kwa kasi na ndipo basi lilipoongeza kasi kubwa
ambayo iliwafanya abiria wote wapige kelele kumtaka dereva apunguze
mwendo, lakini yeye hakusema lolote.
“Mimi nilikuwa nimesimama mlangoni na kondakta wa
gari hilo na hata ajali hiyo ilipotokea sikuiona bali alijikuta nikiwa
kwenye maji hadi nilipookolewa na wasamaria wema.
“Nilipotokea ni kama Mungu tu hakutaka nife…gari
ilipinduka vibaya na wengi wamekufa, jamaa zangu na wengi tulikuwa
tunakwenda kununua bidhaa kwa ajili ya biashara zetu.”
Katika ajali hiyo watu 19 walipoteza maisha na hadi jana maiti 15 kati ya 18 zikichukuliwa na ndugu zao.
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ilifurika umati wa
watu waliokuja kushuhudia na kutambua majeruhi pamoja na kuchukua miili
ya jamaa zao.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Aminiel Ngamuo
alisema baada ya ajali ndugu wa marehemu walimimika juzi jioni
kuzitambua na walifanikiwa kuwatambua ndugu zao huku maiti tatu za
wanaume zikiwa zimebaki hadi jana mchana.
Hata hivyo Dk Ngamuo alishindwa kutaja majina ya waliotambuliwa akisema majina yalifungiwa kwenye ofisi zingine.
Maeneo mengi ya mkoa wa Mbeya yalikuwa na vilio
hasa katika maeneo ya Iyunga, Nzowe, Uyole na Mwanjelwa ambako abiria
hao walitokea.
94 wapoteza maisha Aprili
April 17
Aprili 15
Aprili 12
April 9
April 7
April 3
94 wapoteza maisha Aprili
Jumla ya watu 94 wamepoteza maisha katika matukio
mbalimbali ya ajali zilizotokea kuanzia Aprili Mosi hadi Aprili 17 pekee
nchini.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini chanzo kikubwa
cha ajali hizo ni mwendo kasi wa madereva na ubovu wa miundombinu katika
barabara nyingi nchini.
Miongoni mwa ajali zilizotikisa nchi kwa mwezi April ni kama ifuatavyo:- Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
April 17
Gari ndogo aina ya Toyota Hiace lilitumbukia mtoni
katika eneo la Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kusababisha vifo
vya watu 19.
Katika ajali hiyo walifanikiwa kupona watu wawili
akiwemo utingo huku chanzo chake kikielezwa kuwa ni mwendo kasi wa
kipanya hicho hali iliyosababisha breki kugoma.
Siku hiyo hiyo wachimbaji wadogo 19 wa dhahabu
waliokuwa katika mgodi wa Kalole wilayani Kahama walipoteza maisha baada
ya kufunikwa na kifusi kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
nchini.
Aprili 15
Basi la Air Jordan lilipinduka wilayani Nzega
barabara ya kwenda Igunga, mkoani Tabora na kusababisha kifo cha mtu
mmoja na kujeruhi kadhaa akiwemo mwanamke mmoja aliyekatika mkono.
Aprili 12
Watu 18 waliteketea kwa moto baada ya basi la
Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na
kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Uduzungwa, Morogoro
April 10
Gari aina ya fuso liligongana na powertiller katika kijiji cha Endasak wilaya ya Hanang’ na kusababisha vifo vya watu saba.
Siku hiyo hiyo basi la Nyahunge liligongana na gari ndogo ya Toyota Mark II mkoani Mwanza na kusababisha vifo vya watu wanne.
Mkoani Iringa mtu mmoja (mwanafunzi) alipoteza maisha baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Costa.
April 9
Watu 12 walifariki dunia katika ajali iliyohusisha
magari matatu eneo la Mkata, Kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani
Tanga. Magari yaliyohusika ni mabasi ta Ratco, Shengena na gari dogo
aina ya Passo.
Siku hiyo hiyo basi la kampuni ya Happy Nation
lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Mbeya lilipata ajali na
kusababisha vifo vya watu wawili.
April 7
Watu watatu walipoteza maisha wilayani Butiama baada ya lori kuacha njia na kuwagonga watembea kwa miguu.
April 3
Gari aina ya Toyota Coastal lililokuwa limebeba
mashabiki wa Simba waliokuwa wakielekea Kagera lilipata ajali katika
eneo la Makunganya mjini Morogoro na kusababisha vifo vya watu saba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment