Sunday, April 19, 2015

USALAMA WAIMARISHWA AFRIKA KUSINI

Ubaguzi dhidi ya wageni nchini Afrika kusini 
 
Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika maeneo yenye mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini.

Rais Jacob Zuma amewatembelea watu hao walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo.
Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita.

Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini. Nchini Harare Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alilaani ghasia hizo.

Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme mmoja wa Kizulu, Goodwill Zwelethini, kusema kuwa raia wa kigeni sharti waondoke Afrika Kusini. Akiongea katika kambi hiyo iliyoko mjini Durban kiongozi mkuu wa jimbo la Gauteng, David Makhura, anasema kuwa uhasama na ghasia hizo zinazoshuhudiwa, haundamani na uhuru wa miaka mingi ambayo Afrika Kusini ilipigania. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...