Sunday, April 19, 2015

MADEREVA WA MABASI KAMA WA BODABODA...!!!

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akitoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili 12, sawa na siku 102 vifo 969.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akitoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya January Mosi hadi Aprili 12 mwaka huu, sawa na siku 102 vifo 969.

WAKATI ajali za barabarani zikiendelea kumaliza nguvu kazi ya Taifa na kuumiza vichwa vya Watanzania kuhusu suluhisho la ajali hizo, imefahamika moja ya tatizo sugu ni kukosekana kwa madereva wenye taaluma stahiki, ingawa wana leseni.

Wiki hii peke yake, ajali tatu za mabasi zilizotokea Mbeya, Morogoro na maeneo ya Mwanza, zimesababisha vifo vya watu 40 ndani ya siku sita.

Tayari Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ametoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili 12, sawa na siku 102 vifo 969. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kwa upande wa usafiri wa kutumia pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda), Kamanda Mpinga ameeleza kuwa kati ya Januari na Machi, sawa na siku 90 madereva wa bodaboda ambao Serikali ilishakiri kuwa wengi hawana leseni, wamesababisha vifo vya watu 220.

Ujuzi sifuri Akizungumza na gazeti hili wiki hii, mmoja wa wataalamu wa mambo ya usafirishaji nchini, alisema mabasi ya kusafirisha abiria nchini, ni mengi kuliko idadi ya madereva wenye taaluma ya kuendesha abiria.

Mazingira hayo ni sawa na usafiri wa bodaboda, ambao nao unakabiliwa na tatizo kubwa na pikipiki nyingi zilizosajiliwa, kuliko idadi ya madereva wake waliopatiwa leseni.

“Mimi nina uhakika kabisa ajali hizi zina uhusiano mkubwa na mafunzo kwa madereva, kwa kuwa kama dereva angekuwa anapona katika ajali, tungesema amepata mafunzo stahiki, lakini wengi wanakufa kwakuwa hawana mbinu za kupambana na ajali,” alisema.

Alisema ni dhahiri kuwa madereva wa Tanzania hawana ujuzi wa kutumia vyombo hivyo na kufafanua kuwa, vyombo wanavyoendesha vinajulika vinaua, ndio maana katika mafunzo madereva lazima wapewe mbinu ya kujilinda kama inavyofanyika katika nchi nyingine.

Mtaalamu huyo alihoji iweje marubani wa ndege binafsi, zinazobeba abiria wanne hadi sita, wapelekwe katika mafunzo kila baada ya miaka minne, lakini kwa madereva wanaobeba abiria zaidi ya 65, wanakataa kupelekwa mafunzo baada ya miaka mitatu na kuongeza kuwa hapo kuna tatizo lazima liangaliwe.

Alisema madereva wanapaswa kuelimishwa kuwa mafunzo hayo, ndio mwanzo wa kuandaa kanuni za mafunzo kwa madereva, ili watambulike rasmi kama walivyo marubani na manahodha.

Uzoefu nchi nyingine Mtaalamu huyo alisema duniani kote udereva hususan wa abiria, ni kada ya juu inayolipwa mshahara mkubwa, huku mafunzo yake yakiwa magumu na huchukua muda mrefu.

Alitoa mfano wa nchi ya Uingereza, ambako mtihani hufanyika kwa kutumia mtandao wa kompyuta, ambapo kama dereva mtarajiwa akifaulu kwa kupata zaidi la asilimia 70, cheti kinajiprinti chenyewe.
Alisema katika mafunzo hayo, hakuna kujuana bali kompyuta tu zinafanya kazi na hivyo ufaulu wake na kupata cheti au leseni ni halali, kuliko kufanya mtihani kwa kujuana na kupeana leseni.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, mitihani hiyo katika baadhi ya nchi ikiwemo Afrika Kusini na Japan, hata leseni ya gari dogo, dereva lazima afanye mtihani kabla ya kupata leseni.

Katika kompyuta hizo, kuna maswali zaidi ya 5,000 na kila anayetaka kuwa dereva, hutakiwa kujibu maswali 300 ili hata wakiwa wawili, kila mmoja atajikuta akipewa maswali tofauti na mwingine.

Ajira nje Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, madereva wengi wa Tanzania wakijaribu kutafuta ajira nje, hawatapata kwa kuwa kabla ya ajira, watapaswa kufanya mitihani hiyo, ambayo hapa nchini madereva wameonesha kuikataa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na Habari Leo

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...