Monday, April 20, 2015

MBWANA AWATAKA MASHABIKI WA PRISONS KUISAPOTI HADI MWISHO

makata-march6-2015
Mbwana Makata, kocha mkuu wa Tanzania Prisons.
 
MBWANA Makata, kocha mwenye uzoefu wa kufundisha timu za majeshi safari hii amepewa jukumu la kuibakisha Tanzania Prisons ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

Makata, kocha wa zamani wa JKT Ruvu na JKT Oljoro jana ameiongoza Prisons kupata sare nyumbani ya goli 1-1 dhidi ya Wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa CCM Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Baada ya sare hiyo, Makata amesema: “Mechi ilikuwa ni muhimu kwetu kuweza kupata matokeo ya ushindi, lakini mechi ilikuwa ngumu na tumeweza kutapa sare ya goli 1-1. Kikubwa niwapongeze vijana wangu kwasababu ratiba kwetu ilibana wiki hii, tulicheza jumatano, tukawa safarini na kucheza tena leo (jana), muda wa maandalizi haukuwepo."

"Cha msingi niwaombe wakazi wa Mbeya, mashabiki wa Prisons waisapoti timu yao, tupambane mpaka dakika za mwisho tuone nini kitatokea” Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...