Thursday, April 09, 2015

WABUNGE 50 KUHAMIA ACT...!!!

 
Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wahariri wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, yaliyopo Tabata Relini, Dar es Salaam jana.

Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa mwezi uliopita.
Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Akizungumza na waandishi wa Mwananchi katika ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Zitto alisema ACT ni chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya uzinduzi wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho kinaungwa mkono na watu wengi.
“Tuna wagombea ubunge wengi wakiwamo wabunge wa sasa ambao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba hawatagombea kupitia vyama vyao vya sasa. Wapo ambao hawatakwenda hata katika kura za maoni za vyama vyao na wameshafanya uamuzi,” alisema.
Huku akizungumza kwa kujiamini, Zitto alisema wabunge hao ndiyo sababu ya chama hicho kuwa na uwezo wa kujiendesha na kufafanua kuwa ACT kinawakaribisha wabunge na makada wote kutoka vyama vya Chadema na CCM.
“Wale ambao wanabanwa CCM na kukosa uhuru wa kuhoji jambo lolote hiki (ACT) ndicho chama chao. Wale ambao wanaamini kuwa aina za siasa tulizotaka kuzifanya ndani ya Chadema tukashindwa kuzifanya na wanadhani ni siasa muhimu zinazotakiwa, wapo na sisi,” alisema.

Kuhusu Kigoma
“Nahitaji majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT,” alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.
Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.
Alipoulizwa iwapo wabunge hao wa majimbo ya mkoa huo ni miongoni mwa watu watakaohamia chama hicho alisema, “Sasa huo ni mtizamo wenu. Ukiwa mwanasiasa lazima uwe na msingi, nataka msingi uwe Kigoma.

 Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Tutakutana tena kwenye chumba hiki (cha mikutano) baadaye mwezi Novemba ili mnisute kwa kauli yangu na hapo itakuwa baada ya matokeo kutoka. Nahitaji kushinda kila kitu.

Nafasi ya CCM
Akizungumzia nafasi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu alisema: “CCM inaweza kuondoka madarakani katika uchaguzi huu. Unajua chama hiki ilikuwa kiondoke madarakani mwaka 1995 wakati wa (Augustine) Mrema lakini kulikuwa na (Julius) Nyerere ambaye alikuwa na uwezo wa kuzunguka na kusema watu waendelee kuichagua CCM.
“Lakini mwaka 2015 Nyerere hayupo na hakuna mwenye kaliba yake ambaye anaweza kuzunguka na kusema msichague upinzani, chagueni CCM.
“Katika chaguzi za Serikali za mitaa zilizopita, CCM ilikuwa ikishinda kwa asilimia 91 hadi 96, lakini katika uchaguzi wa mwaka 2014 asilimia zimeshuka hadi 75.
Alifafanua kuwa kipindi ambacho CCM ilikuwa ikipata kura nyingi katika uchaguzi wa mitaa katika ubunge ilikuwa ikipata asilimia 60.
Akitolea mfano asilimia ya kura za urais za CCM tangu mwaka 1995 alisema, “Mwaka 1995, CCM ilipata asimilia 61, mwaka 2000 (asilimia 71), mwaka 2005 (asilimia 80) na mwaka 2010 (asilimia 60).
“Kipindi ambacho CCM ilikuwa inapata kati ya asilimia 90 hadi 96 ya uchaguzi wa mitaa katika ubunge ilikuwa inapata asilimia 60. Sasa hivi imepata asilimia 75 Serikali za mitaa unategemea nini katika Uchaguzi Mkuu? Hiki ni kiashiria kwamba hali ni mbaya kwa CCM.”

Alisema changamoto iliyopo ni uwezekano wa kupata rais ambaye chama chake kitapata wabunge wachache na hivyo kushindwa kupata waziri mkuu kwa mujibu wa Katiba.
“Kuna uwezekano wa kuwa na rais kutoka upinzani na waziri mkuu kutoka CCM.”
Alisema vyama vya upinzani vinaweza kutoa rais lakini haviwezi kupata viti vingi vya ubunge kwa sababu vyama hivyo vinapata ushindi zaidi katika majimbo ya mijini na miji midogo ambako watu wanataka mabadiliko na siyo katika majimbo ya vijijini ambako watu wanachagua mtu kwa uwezo wake wa fedha na umaarufu wake.
“Jambo hilo likitokea itakuwa ni changamoto ya kikatiba kwa sababu chama chenye wabunge wengi ndicho kinakuwa na waziri mkuu, lakini Katiba inasema waziri mkuu anateuliwa na rais.
Rais anatakiwa kumteua waziri mkuu kutoka chama chenye wabunge wengi na Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais.
Ikitokea hivyo, rais anachoweza kukifanya ni kuvunja Bunge ili kurudi katika uchaguzi,” alisema.
Alisema ili kuepuka jambo hilo, lazima upinzani umtangaze mtu atakayekuwa waziri mkuu iwapo utashinda jambo ambalo alisema siyo maarufu katika siasa za Afrika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...