Wananchi
wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa kumi tangu kutokea kwa
tetemeko la ardhi lililosababisha mawimbi makubwa katika bahari ya
Hindi, tsunami na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watu laki mbili na
elfu ishirini katika eneo kubwa.
Umati wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la tsunami katika eneo la Banda Aceh katika kisiwa cha Sumatra.Mji huo ulisambaratishwa kabisa na tetemeko kubwa la ardhi na mawimbi ya tsunami. Makamu wa Rais wa Indonesia(Jusuf Kalla) anaongoza maadhimisho hayo na atawashukuru wafanyakazi wa kujitolea katika eneo hilo na duniani kote kwa kulisaidia eneo la Aceh kurejea katika hali ya kawaida baada ya mkasa huo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.