Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) umesema kuwa Rais Jakaya Kikwete na CCM hawaeleweki
ukidai ni kutokana na kukiuka makubaliano yao kuhusu kuendelea kwa Bunge
Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
Umoja huo pia umedai kwamba Mahakama Kuu ya
Tanzania imeshindwa kutoa uamuzi fasaha kuhusu tafsiri ya kisheria ya
mamlaka ya Bunge hilo katika kurekebisha Rasimu ya Katiba kwa kuogopa
lawama kutoka Ukawa na CCM.
Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP, NLD
na NCCR-Mageuzi ulieleza hayo jijini hapa jana ulipozungumzia Mchakato
wa Katiba ulipofikia, hasa baada ya Bunge hilo kufanya marekebisho ya
kanuni kwa wajumbe wake kuruhusiwa kupiga kura kwa njia ya mtandao.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa makubaliano ya
kusitishwa kwa Bunge hilo kati yao na Rais Kikwete yameshindwa
kutekelezwa, jambo ambalo wanashindwa kuelewa sababu zake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz