Idadi
ya raiya kutoka Uropa wanaojiunga na kundi la wapiganaji wa Kiislamu
nchini Syria na Iraqi imeongezeka hadi zaidi ya 3,000 kulingana na mkuu
wa kitengo cha kupambana na ugaidi bara la ulaya.
Gilles de
Kerchove ameonya kuwa mashambulizi ya hewa yanayofanywa na nchi za
Magharibi yataongezea hatari ya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika
bara la Ulaya.
Vikosi vikiongozwa na Marekani vimetekeleza
mashambulizi ya hewa mia mbili dhidi ya wanamgambo wa Islamic state wa
Iraqi tangu Agosti na Jumatatu iliyopita wakaanza kulenga wale walioko
Syria.
Bunge la Uingereza litapiga kura kwa mashambulizi ya hewa dhidi ya Iraqi siku ya Ijumaa.
Kundi la IS wameteka sehemu kubwa za Syria na Iraqi katika miezi ya hivi karibuni.
CIA inakisia kuwa kundi la IS linaweza kuwa na wapiganaji mpaka 31,000 huko Iraq na Syria, mara tatu zaidi ya wale waliohofiwa.
Mashambulizi haya
yaliotekelezwa siku ya Alhamisi na ndege za Marekani, Saudi na UAE
zilikuwa zinalenga mitambo 12 ya kusafisha mafuta nchini Syria .
Msemaji
wa Pentagon Rear Admiral John Kirby alisema kuwa kusudi la mashambulizi
haya ya hewa halikuwa kuwaua wanamgambo hao lakini ilikuwa kuharibu
maeneo ambayo yalikuwa yakiletea kundi hilo fedha kupitia soko nyeusi.
Baadaye,
siku ya Ijumaa, wabunge wa Uiungereza wataulizwa kuunga mkono
mashabulizi dhidi ya wanamgambo wa IS Iraqi lakini sio Syria. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment