Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwisigwa alisema jana kuwa suala hilo lipo kisheria zaidi.
“Kama kweli Simba, Yanga wamechezesha wachezaji
wasio na vibali vya kufanya kazi nchini ni kosa na Serikali, inaweza
kuwachukulia hatua klabu na wachezaji wao,” alisema Mwesigwa.
Hata hivyo, alisema kuwa adhabu ya kunyang’anywa
pointi haielezi moja kwa moja na hadi sasa hakuna timu iliyokwenda TFF
kulalamikia suala hilo.
“Hatuwezi sisi kuzinyang’anya pointi kama hakuna
timu iliyokuja kwetu kulalamika, isitoshe Simba nimezungumza nao leo
(jana) baada ya gazeti kuripoti habari hiyo wakasema tayari wamewaombea
vibali wachezaji na kocha wao, hivyo siwezi kujua nani mkweli, Simba na
Uhamiaji,” alisema .
Juzi, Idara ya Uhamiaji ilitoa tamko kuhusu baadhi
ya wachezaji na makocha wa kigeni wa timu hizo kutokuwa na vibali vya
kufanya kazi nchini na kueleza kuwa tayari imeanza msako wa kuwakamata
watakapoonekana wakijihusisha na mazoezi au mechi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya alisema
makocha wa Yanga, Leonardo Neiva na Marcio Maximo na wachezaji Genilson
Santos ‘Jaja’ na Andrey Coutinho bado hawajapata vibali, ingawa tayari
uongozi wa klabu hiyo umewasilisha maombi yao.
Alisema wachezaji wote wa kigeni wa Simba pamoja
na kocha mkuu, Patrick Phiri hawana vibali vya kufanya kazi nchini na
hadi juzi jioni idara hiyo haikuwa imepokea maombi yoyote ya klabu hiyo
kuwaombea vibali hivyo waajiriwa wake hao.
Yanga ilimtumia Jaja kwenye mchezo wa Ngao ya
Jamii hivi karibu dhidi ya Azam, sambamba na kocha Maximo, lakini pia
iliwatumia wachezaji hao kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya
Mtibwa ambayo walifungwa 2-0.
Simba pia iliwatumia wachezaji wake wa kigeni kwenye mechi dhidi ya Coastal Union ambao hawana vibali hivyo.
Emmanuel Okwi ana kibali cha Yanga ambacho kwa
mujibu wa Irovya kinaonyesha kuwa mwajiri wake ni Yanga na wala si Simba
anakocheza sasa.
Rais wa Simba, Evance Aveva alipotafutwa na gazeti
hili jana kutoa ufafanuzi wa suala hilo aligoma kuzungumza na kutaka
atafutwe saa 11.00 jioni na alipotafutwa muda huo hakupokea simu.
“Siko katika ‘mudi’ ya kukujibu swali lako, nitafute baadaye
nitakujibu,” alisema Aveva na kukata simu huku makamu wake, Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ akikataa kulizungumzia suala hilo.
Wakati huo huo, Uhamiaji pia imeanza msako kwenye klabu za Kagera Sugar, Azam, Yanga na Coastal Union ambazo pia zinao wachezaji wa kigeni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kamishna Irovya, alisema oparesheni hiyo itafanyika kwenye klabu hizo zenye wachezaji na makocha wa kigeni.
“Tunachokita ni sheria kuchukua mkondo wake,
tayari tumewasiliana na Uhamiaji Kagera ili kutupa taarifa juu ya kocha
wa Kagera Sugar kufanya kazi hapa nchini na wakati wowote kuanzia sasa
tutakuwa tumepata majibu ya hilo, mbali na Kagera kuna hii timu ya
Coastal Union wao waliomba vibari vya muda mfupi kwa wachezaji wao wa
kigeni ambavyo vinakwisha Desemba 16 mwaka huu.
Ligi Kuu Bara itaendelea wikiendi hii katika viwanja mbalimbali.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment