Siku tatu kabla ya
Bunge la Katiba kuanza kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa,
watu wasiojulikana wameanza kusambaza vitisho vya kuwatia hofu wajumbe
wa Bunge hilo.
Watu hao wamesambaza vipeperushi katika maeneo
mbalimbali ya mji wa Dodoma usiku wa kuamkia jana, wakiwataka wajumbe
kutoingia bungeni vinginevyo yatakayowapata watajuta, huku wajumbe
kutoka Zanzibar wakitishiwa kwa ujumbe wa simu kupitia mtandao wa WhatsApp.
Tayari, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Ali Idd ametoa kauli kuhusu vitisho hivyo akisema Serikali
itachukua kila hatua kuhakikisha wajumbe kutoka visiwani humo ambao
wamekuwa wakipokea vitisho wanakuwa salama.
Mbali na kusambazwa kwa karatasi hizo, maandishi
mekundu yamechorwa katika kuta za jengo la Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma yakisomeka, “No Katiba. No ufisadi.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Vikaratasi vilivyosambazwa vinasomeka: “Onyo.
Dodoma si mahali pa kufuga wezi wa fedha za umma. Utakayeingia bungeni
kuanzia kesho (leo), yatakayokupata utajuta.”
Mkazi wa Dodoma, Sospeter Samwel alimwambia
mwandishi wetu jana kuwa aliokota baadhi ya vipeperushi hivyo jana saa
moja asubuhi katika eneo maarufu la kuuzia magazeti linalotazamana na
Jengo la CCM.
“Tulikuta hayo makaratasi yametupwa tu ovyoovyo
ila baadaye nikasikia maeneo mbalimbali mengine nayo yameonekana
yametupwa. Sijui nani hasa watakuwa wameyasambaza,” alisema.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alipoulizwa jana kuhusu na maandishi hayo alijibu kwa kifupi “No
comment” (sina cha kusema).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime
jana alitoa taarifa ya maandishi kwa wanahabari akisema jeshi hilo
linawasaka watu waliosambaza vipeperushi hivyo.
“Wananchi na wageni wapenda amani waendelee na
shughuli zao kama kawaida kwani polisi tumejiimarisha ipasavyo
kukabiliana na yeyote atakayekiuka sheria na maelekezo yaliyotolewa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi alitoa
onyo kwa watu aliodai wanafanya mzaha akisema vyombo vya usalama viko
macho saa 24. Aliwataka wajumbe kutoa taarifa kwa vyombo vya dola
wanapoona viashiria vya kutokuwa na usalama.
“Kama ng’ombe mzima tumeshakula tumebakiza mkia
tu, niwahakikishie wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, usalama umekuwapo
na utaendelea kuwapo.
Wazanzibari kulindwa
Akizungumzia vitisho hivyo hasa kwa wajumbe kutoka
Zanzibar, Balozi Idd alisema Serikali itachukua kila hatua kuhakikisha
wanakuwa salama.
Alisema kuna ujumbe unazunguka katika mitandao ya
jamii ukitoa vitisho kwa wajumbe wa Bunge hilo na watumishi wa
sekretarieti ya Bunge hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Vyombo vya dola vipo na vitafanya kazi yake.
Vinajua vitisho vyote. Niwahakikishie wajumbe mtakuwa salama na Serikali
itachukua kila hatua kuhakikisha hakuna kitakachotokea.
Hoja 17 za Zanzibar
Akizungumzia kuhusiana hoja 17 ambazo
ziliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman
zenye masilahi ya visiwa hivyo, Balozi Idd alisema kati yake 13
zilikubalika na kubakia nne.
Hata hivyo, alisema baada ya kuangalia zaidi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa waligundua kuwa zilibakia hoja tatu tu.
Alizitaja hoja hizo kuwa ni ibara 86 ambayo inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano atashinda kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50.
Hata hivyo, alisema waliona kwenye Katiba ya sasa
jambo hilo liko kimya kidogo endapo itatokea mgombea hakupata kura
upande wa Zanzibar.
“Tukaona kuwa huyu ni Rais wa Muungano, hivi
asilimia 50 yote apate Bara legitimacy (uhalali) yake kama rais wa
Muungano iko wapi?” alisema na kuongeza kuwa vyema katika Rasimu
ikaingizwa kuwa mgombea huyo pamoja na kwamba anatakiwa ashinde kwa
zaidi ya asilimia 50, basi angalau katiba iweke kiwango fulani cha
kupata upande wa Zanzibar. Alisema baada ya kutafakari ikakubaliwa
Zanzibar angalau mgombea huyo apate asilimia 10 au 15. Hata hivyo,
alisema majadiliano kuhusu suala hilo bado yanaendelea. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment