Klabu ya Azam FC
ndiyo inayoongoza kwa kulipa posho kubwa wachezaji wake kati ya timu
zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa
wachezaji wa Azam ndiyo vinara wa kupata posho zilizoshiba wakizizidi
Yanga na Simba ambao kwa kauli yao wamekubali matokeo.
Mgawanyo huo unaonyesha kwamba Azam kila
inaposhinda mechi moja ya ligi inavuna kiasi cha Sh 4milioni, ambapo
kila mchezaji anapewa Sh130,000 kiwango ambacho ni kikubwa kwa Simba na
Yanga
Kitu kibaya kwa Azam ni pale inapotoa sare au
kufungwa, ambapo hakuna chochote watakaochopata ingawa Simba na Yanga
huambulia kitu zikitoka sare.
Hata hivyo, kiutaratibu unaonekana utaratibu
unaotumiwa na Simba ndiyo mzuri kwani wachezaji wake hupata 40 % ya pato
la mlangoni endapo timu hiyo inaibuka na ushindi huku ikiambulia 20%
inapopata sare katika michezo yao.
Yanga, ambayo hivi karibuni wachezaji wake
waliwasilisha maombi maalumu juu ya kutaka kubadilishiwa viwango vya
posho, mpaka sasa wanaambulia kiasi cha Sh70,000 kila mchezaji kwa mechi
wanayoshinda na hupata Sh 30,000 wanapopata sare.
“Hatuwezi kushindana na Azam, unajua Azam hata
kama haupo katika orodha ya wachezaji wanaocheza mechi, Sh130,000 ipo
palepale, lakini Simba na Yanga haipo hivyo, mchezaji anayecheza mechi
anapata zaidi ya yule aliyekosa mechi,” alisema mmoja wa mabosi wa Simba
ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment